Thursday, June 23, 2016

Mavoko: Nitakipiga Brush Kimombo Changu, Sitaki Kuumbuka Kama ilivyonitokea London

Kiingereza ni lugha inayotupa tabu Watanzania wengi na hakuna anayebisha kuwa kimekuwa kikitukosesha fursa nyingi za kimataifa au kujikuta tukiumbuka.
Rich Mavoko ni mmoja wao na amesema atalazimika kufuata njia ya bosi wake, Diamond ili kujinoa zaidi kuepuka kuumbuka siku za usoni.

“Mwaka jana nilienda London, nikakutana na mtu anaongea Kiingereza pale pale lakini mbona kuna vitu sivielewi anavyoongea, alikuwa ni mhindi ambaye amezaliwa kule kule. Anaweza kuuliza maswali mengi ukaelewa matatu,”
“Kizuri ambacho mimi nakijua usilete mbwembwe jibu unachokielewa kwa time aliyokuuliza, kwahiyo kuna umuhimu sana kwasababu hatuwezi kufika bila kujua hicho kitu,” ameongeza.

Rich Mavoko ana elimu ya kidato cha nne na amedai kuwa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu za kiuchumi.

Diamond naye amewahi kusimulia jinsi alivyowahi kuumbuka miaka kadhaa iliyopita wakati Kiingereza chake kilikuwa cha kuchechemea hali iliyomfanya apate hasira ya kujifunza. Leo hii hitmaker huyo anakipiga kimombo kama kawaida!

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta