Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Thursday, November 10, 2016

Wanafunzi hewa 65,198 wabainika shule za msingi, sekondari nchini

Jumla  ya wanafunzi hewa 65,198 wamegundulika kuwepo katika shule za msingi na sekondari nchini, ambako idadi ya wanafunzi hao isingebainika kiasi cha Sh milioni 931.3 zingepelekwa shuleni kuhudumia wanafunzi hewa kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema kati ya wanafunzi hao wa shule za msingi ni 52,783 na sekondari ni 12,415.

Simbachawene alisema kazi ya uhakiki wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari ilifanyika mikoa yote nchini kutokana na agizo la Ofisi ya Rais, Tamisemi kwa makatibu tawala wa mikoa yote ya Tanzania Bara.

Alisema waliagizwa kuhakiki idadi ya wanafunzi katika shule zote za msingi na sekondari kwa kulinganisha taarifa ilivyokuwa Machi mwaka huu wakati wa ujazaji wa madodoso ya takwimu za shule za awali, takwimu za shule za msingi, sekondari na nyaraka za mahudhurio ya wanafunzi.

Alieleza kuwa taarifa za idadi ya wanafunzi kabla ya kuhakiki Machi 2016, zilionesha kulikuwa na wanafunzi 9,746,534 wa shule za msingi na wanafunzi 1,483,872 wa shule za sekondari.

“Baada ya uhakiki tuliofanya Septemba mwaka huu, inaonesha kuwepo wanafunzi 9,690,038 wa shule za msingi na wanafunzi 1,429,314 wa shule za sekondari,” alieleza na kuongeza kuwa uchambuzi umeonesha kuwa wanafunzi 52,783 wa shule za msingi na wanafunzi 12,415 wa sekondari hawakutolewa maelezo ya uwepo wao shuleni.

Alisema kwa tafsiri rahisi hao ni wanafunzi hewa kwa shule za msingi na sekondari nchini, ambao idadi hiyo ya wanafunzi hewa kama isingebainika kwenye uhakiki huo na kupelekwa fedha, Sh milioni 931.3 zingepelekwa shuleni kuhudumia wanafunzi hewa katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema kati ya fedha hizo Sh milioni 527.8 ni kwa shule za msingi na Sh milioni 403.4 ni kwa shule za sekondari.

Aliitaja mikoa inayoongoza kuwa na wanafunzi hewa ni Tabora (12,112), Ruvuma (7,743), Mwanza (7,349), Dar es Salaam (4,096), Kagera (4,763), Rukwa (4,054), Singida (3,239), Kilimanjaro (2,594), Kigoma (2,323), Njombe (2,307), Simiyu (2,081) na Arusha (1,923).

Mikoa mingine ni Mara (1,855), Tanga (1,378), Geita (1,281), Morogoro (1,172), Mtwara (882), Mbeya (786), Shinyanga (695), Songwe (512), Manyara (330), Dodoma (284), Lindi (281), Pwani (187), Iringa (161) na Katavi (0).

Waziri huyo alisema wanafunzi hewa walianza wakati serikali ilipoanza kupeleka fedha shuleni kama ruzuku.

Alisema Sh bilioni 27 zimekuwa zikipelekwa kila mwezi kama ruzuku ya uendeshaji shule za msingi na sekondari na posho ya madaraka kwa ajili ya wakuu wa shule na walimu wakuu, lakini baadhi ya walimu waliamua kuongeza idadi ya wanafunzi ili wapate fedha zaidi.

“Huu ujinga unaweza kufanywa hata katika ngazi ya wizara ni jambo la uchunguzi, zile fedha hazipiti Tamisemi zinakwenda moja kwa moja shuleni,” alieleza na kuongeza kuwa hatua za kinidhamu zinaendelea kuchukuliwa kwa wale wote waliosababisha uwepo wa wanafunzi hewa na Tamisemi inaendelea kuhakiki takwimu zilizowasilishwa.

“Serikali haitegemei tena kuwepo suala la wanafunzi hewa. Naagiza makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na wakuu wa shule kuhakikisha suala la wanafunzi hewa halijitokezi tena katika shule zote za msingi na sekondari,” alibainisha Simbachawene.

Wednesday, November 9, 2016

Ushindi wa Trump Waacha Kilio Bungeni Dodoma


Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema wabunge wanawake wamesikitishwa na kushindwa kwa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democrat, Hillary Clinton.

Dk. Tulia alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana, baada ya kutambulisha wageni mbalimbali.

Alisema walitarajia mambo yangekuwa mazuri upande wao  akiwa mama (wanawake), lakini haikuwezekana.

“Safari hii haikuwezekana, asikate tamaa maana baada ya miaka minne mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi kuliko ilivyokuwa sasa. Nampa pole mama Clinton kwa kuwa safari hii haikuwezakana,” alisema Dk Tulia huku akishangiliwa na wabunge wanawake na kuongeza:

“Nasikia kuna watu hapa wanasema tungempeleka mheshimiwa fulani… katika maeneo yale mama Clinton angeshinda,” alisema.

Kutokana na kile kilichoonekana kupigwa butwaa na uchaguzi huo, kabla ya kuuliza swali la nyongeza jana asubuhi, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema), alisema ana masikitiko makubwa kwa sababu Hillary Clinton ameshindwa uchaguzi.

“Kwa niaba ya wanawake wenzangu, nampa pole mama Clinton kwa kushindwa uchaguzi, tumeumia sana na tumerudi nyuma,” alisema.

Kauli hiyo ilimfanya Dk. Tulia kumtaka aeleze amepata wapi taarifa wakati bado wabunge wanawake wana faraja  Hillary angeweza kushinda.

Hata hivyo, akijibu swali la Suzan, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Khamis Kigwangala,  alimpa pole Hillary kwa kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Tuesday, October 25, 2016

Rais Magufuli Aongoza Kura Kuwania Tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’

Rais John Magufuli anaongoza  kura za kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’, ambayo hutolewa kwa watu walioonyesha mchango kwa jamii.

Huku zikiwa zimebaki siku 21 kwa mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa, Rais Magufuli anachuana na Rais wa Mauritius,  Ameenah Gulib;  Mwendesha Mashtaka wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela; Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Taifa la Rwanda.

Mpaka jana jioni, Dk Magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 75 likifuata Taifa la Rwanda na nafasi ya tatu alikuwa Madonsela wa Afrika Kusini.

Rais Magufuli anayetimiza mwaka mmoja madarakani wiki ijayo, utendaji wake umeonekana kuwagusa wananchi wa kipato cha chini, hasa kwa falsafa yake ya Hapa Kazi, uwajibishaji na mikakati yake ya kubana matumizi ili kuokoa fedha kwa kuzuia sherehe zisizo na tija.

VIDEO:Majambazi Wenye Pikipiki Wapora $40,000 Ofisini Kwa Mohamed Ishaq (Scandinavia)

Jamaa katika Nissan kaibiwa usd 40,000 na majambazi ofisini kwa Mohamed Ishaq (scandinavia)

Majambazi walimfuatilia tokea benki.

Video ya pili inaonesha tukio lililochukuliwa na rekodi za cctv camera


Wednesday, October 19, 2016

Video: Godbless Lema Avuruga Hotuba ya RC Gambo

Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amepinga vikali hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo la Burka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Hayo yametokea leo Oktoba 18, 2016 ambapo shughuli hiyo ilisimama baada Lema kuvuruga hotuba hiyo na kuipinga vikali akidai imejaa upotoshwaji na siasa ndani yake.

Lema alikuwa akipaza sauti kubwa akisema yeye ndiye aliyetafuta eneo hilo la ujenzi kutoka kampuni ya Mawala Advocate. Bofya hapa kutazama video 

Sunday, October 16, 2016

Afande Aitolea Ufafanuzi Picha Aliyopiga na Makamu wa Rais Samia Baada ya Watu Kudhani Ameondoka ACT


Kitendo cha Afande Sele kupiga picha weekend hii akizungumza mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani Morogoro, kiliibua tetesi katika mitandao ya kijamii zikidai huwenda mwanachama huyo wa ACT amekitosa chama hicho.
afande
Afande Sele akiwa mbele ya msafara wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan

Mwanahiphop huyo ambaye aligombea ubunge katika uchaguzi uliyopita kupitia ACT Wazalendo, wiki moja iliyopita alionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa chama chake.

Jumamosi hii baada ya watu kuona picha hiyo na kudhani amekitosa chama cha ACT, aliandika

Aisee Watanzania sisi wengi wetu hata sijui nani katuloga kiasi cha kufunga kabisa uwezo wetu wa kufikiri nakushindwa kutofautisha hata vitu vidogo na vya kawaida sana vinavyotokea ktk maisha yetu ya kila siku…hebu tazama hiyo picha utaona mimi nipo na makamu wa rais,mkuu wa mkoa wetu na viongozi wengine wa serekali,hiyo inamaanisha kwamba hapo niliitikia wito wa serekali sio wito wa chama chochote cha siasa kitu ambacho hata viongozi au wabunge wa upinzani hufanya hivyo kwasababu serikali na viongozi wake ni mali yetu sote kama raia wa Tz sio mali ya chama fulani hata kama viongoz hao wametokana na chama hicho lkn wakishachaguliwa na wananchi wakapewa dhamana ya kuongoza tayari wanakua ni viongoz wa watu wote ktk taifa sio viongozi wa watu wa chama chao tu,sasa nashangaa pale mtu mmoja kwa sababu ya uvivu tu wakufikiri au labda kwa makusudi tu anaamua kuambukiza uvivu wake huo wa kufikiri na kutofautisha mambo kwa watu wengine…mimi nimeitikia wito wa serekali’mamlaka’ninayoamrishwa kuyatii hata ndani ya vitabu vitakatifu sio chama…lkn pia ktk hali ya kawaida tu ninani mwenye utimamu wa akili ktk taifa lolote awezae kukaidi wito wa makammu wa rais ambae ni sawa na rais wa taifa lake?lkn hata kama ingekua kweli mimi nimehama chama ingawa sifikirii kufanya hivyo bado yangebakia kuwa ni maamuzi yangu na yangepaswa kuheshimiwa…nyongeza ni kwamba hata yule mgombea urais wa marekani kupitia chama cha Republican mr donald trump siku za nyuma alikua ni mwanachama mtiifu wa chama cha mpinzani wake bibi clinton cha democratic na maisha yanaendelea..watz tujifunze maana ya maisha halisi tusijenge taifa la uzushi,fununu na kupakaziana…muwe na j’pili kareem akina ndugu nyote!

Saturday, October 15, 2016

Tazama Video DC Richard Kasesela Akionyesha Jinsi ya Kushika Bunduki na Kupambana na Adui Katika Vita

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akionyesha jinsi ya kushika bunduki na kupambana na adui uwapo katika uwanja wa mapambano.

Ushikaji wa bunduki wakati wa pambano huwa ni changamoto kwa sababu usipokuwa umejiweka sawa ukifyatua risasi kutokana na msukumo unaweza kuanguka.

Katika video hii, baada ya DC Kasesela kumaliza anapongezwa na Wanajeshi waliokuwa katika mazoezi hayo kwa namna alivyofanya vizuri. Itazame video hapa chini. 


Picha za Samaki Aina ya Nyangumi Aliyekufa Ufukweni Bahari ya Hindi Kilwa

Samaki mkubwa amekutwa amekufa jana katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari ya Kilwa, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.

Wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa samaki huyo alianza kuonekana kuanzia jana akielea baharini lakini hawakujua kama alikuwa amekufa hadi leo aliposukumwa hadi kwenye ufukwe wa bahari.

Wakazi hao wanaeleza kuwa samaki huyo ana urefu wa futi 30.


Bodi Ya Mikopo Yapitisha Majina 7904 Ya Wanafunzi Waliopata Mkopo

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetangaza awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini watakaopewa mkopo kugharimia masomo yao.
 
Idadi ya wanafunzi ambao tayari wamepitishwa kupata mkopo ni 7,904, hata hiyo imeelezwa kiwango hicho kitaendelea kubadilika kwa kuwa mchakato unaendelea.

Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya ilibainisha kuwa bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zinazotakiwa na majina ya wanufaika wapya ambayo yameanza kutangazwa kupitia tovuti ya bodi hiyo.

 “Kwa kuzingatia mpango mkakati, pia mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2016/17, Serikali imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo,” alisema Manyanya.

Alitaja vigezo vilivyotumika kuwa ni pamoja na vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele.

Manyanya alizitaja fani zilizopewa vipaumbele kuwa ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta na gesi asilia, sayansi asilia na mabadiliko ya tabianchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Katika taarifa yake, Manyanya alisema pia mchakato wa kuwapata wenye sifa za kukopa uliangalia uhitaji wa waombaji, hususan wenye mahitaji maalumu kama walemavu na yatima, ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele na umahiri. 

“Kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao katika vipengele vyote vya mikopo,” alisema.

Akizungumzia mchakato huo, mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo, Abdul Badru alisema unaendelea kufanywa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na timu ya bodi imejigawa katika vikundi ili kuhakikisha mipango inakwenda jinsi inavyotakiwa.

 “Timu ipo kazini na inafanya kazi yake kwa umakini. Kwa sasa majina ya waliochaguliwa kutokana na vigezo yamewekwa, lakini ni wahusika wenyewe au walezi na wazazi ndiyo wanaweza kuyaona kupitia namba zao za usajili wa kidato cha nne. Lakini siku chache zijazo tunaweza kuwataja wakaonekana kwa kila anayehitaji kuyaona,” alisema Badru.

Majina Ya Wanafunzi Waliopata Mkopo Mwaka Wa Masomo 2016/2017----(Awamu ya Kwanza)


Bodi ya mikopo ya elimu ya juu wametangaza majina ya wanafunzi waliopata mkopo 2016/2017 awamu ya kwanza.

Hapa ni link ya kuangalia kama umepata au laah unaandika namba ya form 4 na code walizokupa hapo.

Kumbuka format ya form 4 no. ni s0001.0001.0001 na sio s0001/0001/0001

Link hii hapa http://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/olas/AllocationFreshers

  
Chini limeambatanishwa FILE la Orodha ya Waliopata Mkopo 2016/17  

1.First List Of Loan Beneficiaries For Academic Year 2016/2017. <<Click here>>
  


2.First Year Loan Allocations Breakdown for 2016/17 . <<Click here>>

Thursday, October 13, 2016

Nauli za ATCL zitakazotumika kuanzia Oktoba 14 hadi 28


Ndege mbili mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400 zinatarajia kuanza kazi wakazi  wa mikoa ya Mwanza, Arusha na Zanzibar watakuwa wa kwanza kupata ofa.

Ofisa Habari wa shirika hilo, Lilian Fungamtama amesema  safari  mpya za ndege hizo  ikiwamo ya Dar es Salaam - Mwanza, nauli iliyopangwa ni Sh160,000.

Amesema safari za  Dar es Salaam - Arusha nauli yake itakuwa Sh180,00 na Zanzibar - Dar es Salaam ni Sh85,000.

“Ofa hii imetolewa na ATCL kwa safari mpya za ndege hizo,” alisema Fungamtama.

Amesema hakutakuwa na safari ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, lakini itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam -Arusha hadi Zanzibar.

 “Ndege ya kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha ndiyo itakayokwenda kuchukua abiria Zanzibar haitatokea Dar es Salaam moja kwa moja,” alisema.

 Akifafanua kuhusu nauli hizo, Fungamtama alisema nauli  ya kutoka Dar kwenda Kigoma itakuwa katika madaraja mawili ambayo ilikuwapo tangu awali.

Amesema bado ndege hizo hazijaanza safari katika mikoa yote hadi hapo watakapotangaza.

Akizungumzia safari za nje ya nchi, alisema itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam - Hahaya hadi Comorro ambayo nauli yake ni Sh543,950 kwenda na Sh926,650 kwa kwenda na kurudi.

 “Lengo letu ni kutoa huduma nzuri itakayomridhisha kila mteja,” alisema Fungamtama.

VIDEO:Wachina wakamatwa Mtwara, wakutwa wakibadili Expire date kwenye dawa

Watu watano wakiwemo raia wawili wa China na Watanzania watatu wamekamatwa Mtwara kwa kutuhumiwa kubadili tarehe zilizokwisha muda wa matumizi kwenye dawa za kilimo (expire date) ili dawa hizo ziingizwe tena sokoni na kuonekana bado zinafaa kwa matumizi.
Inadaiwa watuhumiwa hawa wamefanikiwa kubadilisha dawa hizo kwenye mabox zaidi ya mia sita ( 600) na kuzifanya zionekane mpya ambapo Kamanda wa Polisi Mtwara amesema Watuhumiwa hao walikamatiwa Nangwanda.
screen-shot-2016-10-13-at-12-29-04-pm
Makachero wa Polisi baada ya kupewa taarifa waliwahi kwenye eneo la tukio na kukuta watu wanne wakikwangua chupa kuondoa nembo iliyoonyesha dawa hiyo ilitengenezwatarehe 28 February 2013 na muda wake wa matumizi umekwisha tarehe 27 February 2016.
Nembo mpya feki waliyoitengeneza Wachina hawa inasomeka dawa imetengenezwatarehe 20 February 2016 na inamaliza muda wa matumizi tarehe 19 February 2019.

U

Wednesday, October 12, 2016

ZITTO Kabwe Kwa Mara ya Kwanza Ampiga Dongo Paul Makonda

Zitto Kabwe ameitupia lawama manispaa ya Kinondoni pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kushindwa kudhibiti tatizo la uchafu katika fukwe za Coco Beach.

Amedai kuwa ni aibu kuwa manispaa hiyo inayoongozwa na chama cha upinzani ndani ya mkoa unaoongozwa na kijana, kushindwa kuhakikisha usafi katika fukwe hizo maarufu.

“Uchafu wa namna hii kwenye Manispaa inayoongozwa na Chama cha Upinzani ni aibu,” Zitto ameandika kwenye picha za fukwe hizo alizoweka kwenye mtandao wa Facebook.

“Lakini ni aibu zaidi uchafu wa namna hii kuwa katika mkoa unaoongozwa Na Mkuu wa Mkoa kijana katika mahala anapopita Kila Siku kwenda nyumbani kwake Na kwenda kazini,” ameongeza.

“Hapa Ni Coco Beach kwenye Mihogo. Hata sheria ndogo tu ya Manispaa ya kuwataka wenye shughuli hapa kusafisha mbele ya eneo Lao ingeweka mahala hapa kuwa safi. Kuna mambo hayahitaji misaada ya wazungu wala Wafanyabiashara. Ni akili za kimaendeleo tu.” 

Waziri Awapa Ahaueni walimu Waliotoa kipigo kwa mwanafunzi Mbeya.


Baada  ya uamuzi wa kuwafukuza vyuo walimu wanne waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo katika Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Mbeya (Mbeya Day), serikali imesema vyuo husika vinaweza kushauri adhabu mbadala iwapo vitajiridhisha kuwepo kwa mazingira tofauti na yaliyozingatiwa kwenye uamuzi wa kuwafukuza vyuo.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo juzi alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya alikokuwa katika ziara kwenye shule mbalimbali mkoani humo.

Profesa Ndalichako alisema uamuzi uliochukuliwa na ofisi yake ulizingatia sheria ndogo zilizotungwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm) zinazoainisha makosa yanayoweza kumfukuzisha chuo mwanafunzi.

Hata hivyo, alisema uamuzi uliochukuliwa unaweza kutazamwa upya na vyuo husika iwapo uzito uliochukuliwa na wizara utaonekana kuwa katika mazingira na uhalisia wa tukio husika.

Walimu wanne waliokuwa kwa vitendo katika shule ya Mbeya Day walifukuzwa vyuo baada ya uamuzi wa serikali kutokana na kuhusika kumpiga mwanafunzi Sebastain Chinguku vibao, mateke na fimbo kwa ukatili Septemba 28 mwaka huu shuleni humo.

Walimu hao walibainika baada ya kipande cha video kusambazwa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni. 

Waliohusika na vyuo walivyokuwa wakisoma ni Frank Msigwa (anayedaiwa kumpiga zaidi mwanafunzi makofi kichwani), John Deo na Sante Gwamaka wote wa DUCE-UDSM, na Evans Sanga wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Akijibu swali la idadi ipi ya viboko inastahili kutolewa kama adhabu kwa mwanafunzi anayekwenda kinyume na maelekezo ya shule yake, Profesa Ndalichako alisema binafsi asingependa mwanafunzi achapwe hata kiboko kimoja lakini hilo linawezekana pale wanafunzi watakapozingatia maadili.

“Adhabu yoyote kwa mwanafunzi inatolewa pale anapokuwa amekwenda kinyume na maadili ya shule yake. Kama wanafunzi wote watazingatia maadili sidhani kama kuna mwalimu atakayempiga mwanafunzi hata kiboko kimoja. Haya yote yanatokea kutokana na wanafunzi kukosa nidhamu,” alisisitiza Ndalichako.

Aliwasihi wanafunzi kuzingatia maadili ya shule yao, akisema ndiyo njia pekee ya kuwawezesha kuishi vyema na walimu wao na pia kufanya vyema kitaaluma na kuwasihi wazazi kuwafundisha watoto wao nidhamu ya kuwaheshimu watu wote, akisema malezi hayo yatawapunguzia walimu adha ya kuishi na wanafunzi watukutu ambao kimsingi wanazorotesha utendaji kazi wao.

Tuesday, October 11, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Octoba 12


 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta