Showing posts with label UTAFITI. Show all posts

Friday, September 16, 2016
Thursday, August 25, 2016
Tabia Tatu Kubwa Zinazoleta Tofauti Kati Ya Tajiri Na Maskini
Posted by
Unknown
Kila kitu kinapoanza kwenye hii dunia huwa kinaanza sawa na kitu kingine. Kwa mfano mimea inapoanza kuchipua yote huanza pamoja lakini utofauti hujitokeza katika kukua kwake kwa kadri siku zinavyokwenda, kwa mingine kuwa mikubwa sana na mingine midogo ya kawaida.
Pia hata wanyama wengine wanapozaliwa iwe swala au simba wote huzaliwa wote wakiwa na nguvu sawa lakini utofauti huanza kujitokeza kwa jinsi wanavyoendelea kukua. Wengine hujikuta wana nguvu zaidi kuliko wengine na wengine hubaki wanyonge wanyonge.
Halikadhalika linapokuja suala la mafanikio mambo pia huwa yapo hivyo hivyo. Hii ikiwa na maana kwamba, kila binadamu amezaliwa sawa na binadamu mwingine. Hakuna binadamu ambaye atasema alikuja duniani akiwa na mafanikio na mwingine akiwa hana. Wote tulizaliwa tukiwa hatuna kitu.
Kama mambo yako hivi, ni nini kinacholeta tofauti hizi kubwa? Kwa nini wengine wawe matajiri na wengine wawe maskini? Je, matajiri wanakipi cha ziada kinachowafanya wafanikiwe? Kimsingi, huwa yapo mambo mengi kidogo yanayosababisha wengine wawe matajiri na wengine kuwa maskini.
Lakini katika makala haya tutaongelea mambo matatu ambayo yanahusiana na tabia ambazo zinaleta utofauti kati ya maskini na tajiri. Ni kweli zipo tabia ambazo matajiri wanazo na huwafanya wao kuwa matajiri kila kukicha. Ni tabia ambazo huwatenga kabisa na maskini na kuwaacha matajiri waendelee kufanikiwa.
Ikiwa utaamua kujifunza na kuzifatilia tabia hizi kwa karibu, uwe na uhakika utajiri utakuwa mikononi mwako muda sio mrefu. Nasema hivyo nikiwa na maana hii, ukitaka kuwa tajiri fanya yale ambayo matajiri wanafanya nawe utafanikiwa na kuwa kama wao.
Hebu kwa pamoja bila kupoteza muda, tuangazie nukta kadhaa, zinazoweza kutuonyesha tabia zinazowatenga kati ya matajiri na maskini.
1. Kuwekeza.
Watu wenye sifa ya utajiri ndani mwao hata kama bado hawajafika huko kwenye utajiri halisi ni wawekezaji wazuri sana. Si watu wa kuridhika na chanzo kimoja cha mapato. Wana vitega uchumi vingi sana ambavyo vinawasaidia kuingiza mapato kwa wingi hata kama wamelala.
Kwa mfano uatakuta wamewekeza kwenye mashamba, mafuta, migodi na maeneo mengine mengi. Hii ni sifa mojawapo kubwa inawatenga maskini na matajiri. Ukiona una kitega uchumi kimoja ujue unajizibia nafasi mwenyewe ya kuelekea kwenye utajiri mkubwa.
2. Kuweka akiba.
Suala la kuweka akiba kwa watu matajiri sio suala la hiari, kwao ni lazima. Angalau huweka asilimia kumi ya kile wanachokipata. Wanajua vizuri akiba hizo ni msaada mkubwa kwa baadae katika suala zima la kuwekeza. Wao katika kuweka akiba ni lazima, na pia hawana mchezo katika hilo.
Kutona na tabia hii, huwafanya wazidi kufanikiwa kila siku na kuwaacha maskini wakibaki kuwa maskini. Ni kitu ambacho unatakiwa kujifunza na kuelewa kwamba, akiba ni jambo la msingi sana kujiwekea kama unataka kuwa tajiri. Vinginevyo acha kuweka akiba, uendelee kubaki kwenye umaskini.
3. Kutoa.
Tabia nyingine inayowatenga watu matajiri na maskini ni ile hali ya kutoa. Watu matajiri ni watoaji wazuri sana wa pesa na mali zao. Hufanya hivi si kwa sababu wanazo nyingi, bali kutoa ni moja ya kanuni kubwa ya mafanikio walioamua kuitumia. Huwezi kufanikiwa sana kama hutoi.
Ieleweke hivi, maskini wanaendelea kubaki kuwa maskini kwa sababu ya uchoyo walionao. Hukumbatia sana walivyonavyo na kusahau kutoa. Kosa hilo huwafanya wazidi kuendelea kuwa maskini siku zote za maisha yao. Ili kuwa tajiri ni lazima kutoa.
Kumbuka, tabia ya kuwekeza, kuweka akiba na kutoa ni moja ya tabia kubwa zinazo watenga matajiri na maskini. Matajiri wanajikuta wakiwa ni watu wakuzifanyia kazi tabia hizo na kuwafanya kuwa matajiri na maskini hubaki na umaskini wao kwa sababu ya kutokuzifanyia kazi tabia hizo. Chukua hatua ya kutenda ili kubadili maisha yako.

Tuesday, August 23, 2016
Saturday, August 20, 2016
Zijue Sababu za Kwa Nini Tunazima Simu Ndege Inapotaka Kupaa na Kutua
Posted by
Unknown
Najua kama ni mtumiaji wa usafiri wa ndege utakuwa ushasikia taratibu za abiria kuzima simu wakati ndege inataka kupaa na kutua ila huenda hukawa hujui sababu kwa nini unatakiwa kufanya hivyo, inawezekana ulishajiuliza usipozima unaweza kusababisha ndege kupata ajali au? jibu ni Hapana, isipokuwa unaweza kusababisha muingiliano wa mawasiliano kati ya rubani na waongozaji.
Vibrations au miungurumo ya simu na vifaa vingine vya electronics vinahusika kwa kiasi kikubwa kuvuruga mawasiliano mazuri kati ya rubani na wanaomuongoza, hivyo huwa tunashauriwa kuzima simu na vifaa vingine vya electronics wakati wa kupaa na kutua kwa ndege. Hiyo ni moja kati ya sababu kuu zilizotajwa juu ya swali la ”Kwanini tuzime simu wakati ndege inaporuka na kutua”?.

Thursday, August 18, 2016
Kama Umesoma au Unasoma Kwa Lengo la Kuja Kupata Pesa; Unaweza Kuja Kujidharau na Kuwa 'Disappointed'
Posted by
Unknown
Kama umesoma[au unasoma], kwa lengo la kuja kupata pesa; unaweza kuja kujidharau na kuwa "disappointed". Kwa sababu huku mtaani kuna watu ni ama la saba au hata la saba hawakumaliza lakini ndio wanaoongoza kumiliki pesa za kutisha. Ukipata nafasi ya kusoma; soma kwa bidii, lakini ni vema ukatambua kuwa [fedha za maana] ni nadra sana kukaa kwenye vyeti. Vyeti vikijitahidi sana vitaishia kukupa pesa ya kubadilishia mboga. Akili inayokupa vyeti madarasani ni tofauti kabisa na akili inayotumika mtaani katika utafutaji wa pesa! #SmartMind
Tuesday, August 16, 2016
Sunday, August 14, 2016
Yajue mambo 10 kuhusu Bundi
Posted by
Unknown
Leo utajua mambo mengi ya kuvutia zaidi kuhusu Bundi
1.Kuna cafe ya Bundi(owl cafe) huko Japan,ambapo unaweza kucheza na bundi huku ukiufurahia mlo mzuri
2.Bundi wa sehemu zenye baridi kali ni wakubwa zaidi wana urefu wa inch 20-27,Bundi mzee zaidi wa sehemu zenye baridi anaweza kuishi hadi miaka 9 na miezi 5
3.Bundi anaweza kukaa mabara yote isipokuwa Antarctica
4.Bundi wanaweza kula hadi panya 1000 kila mwaka, wengi wa aina hii ya bundi wanatumiwa na wakulima kudhibiti idadi ya panya mashambani
5.Bundi anaweza akamla Bundi mwenzie,inategemea na ukubwa wa bundi na bundi, Bundi mkubwa anaweza kumla bundi mdogo wa aina nyingine.
6.Kwa aina tofauti za Bundi,majike ni makubwa,mazito na yana fujo zaidi ya madume
7.Bundi wanaona vitu vya mbali,hawawezi kuona vitu vilicho karibu nao.
8.Watu wanaweza kuokoa maisha ya watoto wa Bundi wajane,kwa kuwapa mdori mkubwa wa Bundi. Katika zoo moja huko southhampton, watoto wa Bundi wanaamini dori kubwa waliowekewa kuwa ni mama yao na uwa wanaenda kujikunyata chini ya mabawa ya huo mdori wakijisikia baridi
9.Rekodi za Bundi zilikuwapo toka zamani sana, Bundi mkubwa zaidi katika rekodi alikuwa na urefu wa ft 3
10.Ndege huyo anatumika sana na tamaduni nyingi kwa imani za kishirikina

Subscribe to:
Posts (Atom)