Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Wednesday, October 12, 2016

ZITTO Kabwe Kwa Mara ya Kwanza Ampiga Dongo Paul Makonda

Zitto Kabwe ameitupia lawama manispaa ya Kinondoni pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kushindwa kudhibiti tatizo la uchafu katika fukwe za Coco Beach.

Amedai kuwa ni aibu kuwa manispaa hiyo inayoongozwa na chama cha upinzani ndani ya mkoa unaoongozwa na kijana, kushindwa kuhakikisha usafi katika fukwe hizo maarufu.

“Uchafu wa namna hii kwenye Manispaa inayoongozwa na Chama cha Upinzani ni aibu,” Zitto ameandika kwenye picha za fukwe hizo alizoweka kwenye mtandao wa Facebook.

“Lakini ni aibu zaidi uchafu wa namna hii kuwa katika mkoa unaoongozwa Na Mkuu wa Mkoa kijana katika mahala anapopita Kila Siku kwenda nyumbani kwake Na kwenda kazini,” ameongeza.

“Hapa Ni Coco Beach kwenye Mihogo. Hata sheria ndogo tu ya Manispaa ya kuwataka wenye shughuli hapa kusafisha mbele ya eneo Lao ingeweka mahala hapa kuwa safi. Kuna mambo hayahitaji misaada ya wazungu wala Wafanyabiashara. Ni akili za kimaendeleo tu.” 

Monday, September 19, 2016

Ujumbe wa Zitto Kabwe kwa Rais Magufuli kuhusu sakata la ESCROW

Kwanini Rais Magufuli hafanyii Kazi suala la IPTL?

Matapeli hawa wataendelea kuipa hasara Nchi yetu mpaka lini? Sasa mahakama ya ICSID imeamua kuwa Benki ya Standard Chartered ilipwe Shilingi za Kitanzania Bilioni 300 na riba. TANESCO wanaingia Hasara hii Kwa sababu ya wizi wa Fedha za TEGETA Escrow, na Rais bado anavuta miguu kuchukua hatua dhidi ya suala hili. Nini kimemkuta Rais Magufuli? Rais anataka tuamini kuwa IPTL/PAP Ni kweli waligharamia Mkutano Mkuu wa CCM uliompa yeye Uenyekiti ?

Tanzania hapo ni hasara tupu:

1) Mmelipa matapeli Fedha zilizokuwa kwenye TEGETA escrow account

2) Mmewapa mtambo wa kuzalisha umeme matapeli hao na mnaendelea kuwalipa capacity charges mpaka sasa

3) Mnawalipa standard chartered Fedha zao Kwa mtambo ambao sio wenu na Kwa Fedha ambazo mngezitoa escrow a/c lakini sasa mtazitoa hazina

Rais achukue hatua zifuatazo

– Awafikishe mahakamani watu wote waliohusika na kuitia Nchi hasara katika sakata la TEGETA Escrow
– Aitwae mitambo ya IPTL kisheria na kuimilikisha Kwa TANESCO
– Amkamate Bwana Harbinder Singh Seth na wafuasi wake wote na kuwafikisha mahakamani Kwa makosa ya utapeli, wizi, uhujumu uchumi, utakatishaji wa Fedha nk
– Benki iliyotumika kupitisha Fedha za TEGETA escrow ndio ilipe Hilo deni tunalotakiwa kulipa

Rais aamue kusimama na watanzania au kusimama na matapeli wa TEGETA escrow

Thursday, September 15, 2016

Utafiti wa Twaweza: Watazania 96% wanampongeza Rais Magufuli

Taasisi inayojishughulisha na kufanya tafiti mbalimbali nchini ya TWAWEZA. Leo imetoa ripoti inayoonyesha kuwa asilimia 96 ya Watanzania wapongeza utendaji wa Rais Magufuli, huku asilimia 68 wapongeza uwajibikaji wa wabunge wao.

Aidha katika ripoti hiyo inabainisha kuwa jambo maarufu alilofanya Rais Magufuli ni uondoaji watumishi hewa huku zuio la kuingiza sukari likikosa umaarufu.

Kiwango cha kukubalika cha Rais Magufuli katika utafiti mpya ni cha juu kuliko marais 128 wa Afrika.

Monday, September 5, 2016

Ufafanuzi wa ACT- Wazalendo Kuhusu Taarifa ya Pro Lipumba Kujiunga na Chama Hicho

Baada ya kumalizika kikao cha kamati kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika leo septemba 05/2016 jijini Dar esSalaam

Kesho Jumanne Septemba 06/2016,Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo watakutana na waandishi wa habari na kuelezea masuala mbali mbali muhimu yanayoendelea sasa ikiwemo:
• Hali ya Uchumi wa Taifa
• Hali ya Kisiasa ya Taifa
• Hatari ya Kuvunjika Kwa Umoja wa Kitaifa

Wapi:Makao Makuu ya ACT wazalendo yaliyopo Sayansi Kijitonyama jirani na Kanisa la KKKT

Muda:Saa tano kamili asubuhi (11:00am)

Kuhusu taaarifa zilizosambaa za Prof. Lipumba kujiunga na chama hicho, ACT- Wazalendo wamesema kuwa hawana taarifa yoyote ya Prof. Lipumba kujiunga na chama hicho na pia kikao cha leo hakihusiani na ajenda yoyote ya kupokea wanachama.

Muhimu kuzingatia muda

Abdallah Khamis
Afisa Habari
0655549154

Thursday, September 1, 2016

Vifaa Vyote vya Freeman Mbowe Vilivyokamatwa Jana na NHC Vitauzwa Baada ya Siku 14 Ili Kufidia Deni Analodaiwa



VIFAA vilivyokamatwa jana vya klabu ya usiku ya Bilicanas na ofisi ya gazeti la Tanzania Daima, vyote vinavyomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, vitapigwa mnada na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) siku 14 kuanzia jana, endapo atashindwa kulipa Sh. bilioni 1.2 za deni la pango la miaka 20.

Mbowe alikuwa mpangaji katika jengo la NHC lililopo makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Vyombo hivyo vilikamatwa jana na kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyopewa kazi ya kuondoa vifaa hivyo baada ya Mbowe kushindwa kulipa deni hilo ndani ya miezi miwili ya notisi ambayo shirika hilo lilikuwa limempatia.

Meneja wa Kitengo cha Kukusanya Madeni kutoka NHC, Japhet Mwanasenga aliyekuwa akisimamia ukamataji wa vyombo hivyo, alisema Mbowe ana muda wa wiki mbili kuanzia jana kulipa deni la Sh. bilioni 1.172 vinginevyo vitapigwa mnada.

Vifaa vilivyokamatwa ni pamoja na kompyuta, meza na viti.

Alisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kumuondoa mteja wao, ikiwamo notisi na kwamba vifaa hivyo vitashikiliwa kwa muda huo wa wiki mbili.

“Tunashikilia vyombo kwa muda wa wiki mbili na iwapo atashindwa kulipa vitapigwa mnada na dalali, (mdaiwa) akishindwa kulipa anapangishwa mwingine,” alisema.

Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa majengo yake hivyo mteja ambaye anadaiwa ajiandae kuondolewa wakati wowote na kwamba zoezi la jana ni mwanzo tu.

Baadhi ya watu wamelihusisha tukio la kuondolewa Mbowe katika ofisi hizo na masuala ya kisiasa.

Lakini Mwanasenga alisema uamuzi wa kumuondoa ofisi hizo hauna uhusiano na masuala ya kisiasa.

Alisema wapangaji wa jengo hilo wapo wengi pamoja na wadaiwa na kwamba baada ya mchakato huo kuanza mdaiwa yeyote atakayeshindwa kulipa kodi ataondolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari katikati ya wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15.

Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanaa pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa, Mchechu alisema. Notisi hiyo ilikuwa inaisha juzi.

Alisema baada ya muda huo kumalizika, utekelezaji wa kuondolewa katika majengo hayo utaanza ukiambatana na uchukuaji wa hatua za kisheria.

Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadiawa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.

Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma.

"Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma," alisema Mchechu, hivyo "fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo."

Alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwa ujenzi wa nyumba za watumishi 300 hadi 500 mkoani Dodoma.
 
Alisema ujenzi huo unatarajia kuanza mara moja na utachukua miezi 12.

Kwa mujibu wa Mchechu, Sh. bilioni 60 za ujenzi wa nyumba hizo zitatokana na fedha za ndani.

Alisema shirika hilo limenunua ekari 240 eneo la Iyumbu, ekari saba Chamwino, nne Bahi na Chemba ekari nne pia ikiwa ni kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano kuhamia Dodoma.

Alisema fedha nyingine zitapatikana baada ya nyumba 97 za shirika hilo zilizopo Medeli mjini Dodoma kuuzwa.

UVCCM yaivaa rasmi Chadema kwa kushindwa kufanya Maandamano ya UKUTA

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umewavaa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile walichodai kuendesha siasa za maigizo baada ya kushindwa kuzindua Operesheni UKUTA, Septemba 1.

Kupitia taaria yake kwa vyombo vya habari, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, amesema kuwa Chadema walijua kuwa hawana ubavu wa kufanya maandamano na mikutano nchi nzima Septemba 1 na kwamba walichofanya ni kuwatia hofu wananchi.

“UVCCM tulijua, tulielewa na kutambua bayana kwamba Chadema walikuwa wanafanya maigizo katika siasa, hawana ubavu wala jeuri ya kuandamana kwa madai ya kipuuzi na ambayo sio ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu,” alisema Shaka.

Aidha, Shaka alikanusha sababu zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuahirisha maandamano hayo kuwa wameombwa na viongozi wa dini ili waweze kukaa na pande zote kujaribu kutafuta suluhu kwa amani.

“UVCCM inatamka bayana kuwa hakuna majadiliano, mazungumzo wala mijadala itakayojadiliwa kati ya Serikali ya CCM na Chadema. Tunaomba Serikali ya Rais John Magufuli iendelee na mikakati yake ya kisera,” Shaka ameongeza.

Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alisisitiza kuwa Chadema hawana ubavu wa kufanya maandamano na mikuano nchi nzima Oktoba 1 kama walivyosema, baada ya kushindwa kufanya hivyo Septemba 1.

Shaka amesema wanachokifanya hivi sasa Chadema kinatokana na kushindwa kubuni mikakati ya kufanya siasa ili chama chao kiimarike na kukubarika.

Juzi, Chadema walitangaza kuahirisha uzinduzi wa oparesheni UKUTA nchi nzima, iliyokuwa imepangwa kufanyika jana (Septemba 1) kwa maandamano na mikutano nchi nzima.

UVCCM pia walitangaza kuahirisha maandamano yao ya nchi nzima waliyokuwa wamepanga kuyafanya Agosti 31 kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi aliyoifanya ndani ya kipindi kifupi.

Maandamano ya pande zote mbili yalipigwa marufuku na Jeshi la Polisi nchini.

[VIDEO]BREAKING NEWS::ALICHOKISEMA PROF LIPUMBA BAADA YA KUVULIWA UANACHAMA NA KIKAO KIKUU CHA CUF HUKO ZANZIBAR.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI NIMEKUWEKEA LIVE KABISA.



HIZI NDIZO NJIA RAHISI ZA KUMRIDHISHA MSICHANA WAKO ZIONE HAPO CHINI

Wednesday, August 31, 2016

VIDEO: Alichokiongea RC Makonda Kuhusu September 1

August 30 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wananchi kuungana na Jeshi la Wananchi Tanzania katika maadhimisho ya miaka 52 ambayo yatafanyika September 1 2016.
Katika maadhimisho hayo Jeshi la Wananchi pamoja na wananchi wenyewe wataitumia siku hiyo kuchangia damu salama pamoja na kufanya usafi wa jiji.
Lakini RC Makonda amewataka wana Dar es salaam wote pamoja na watanzania kwa ujumla kuondoa hofu ya kuwepo kwa maandamano yanayoitwa ‘UKUTA’

Unaweza kuendelea kumsikiliza RC Makonda kwenye hii video hapa chini… 

Monday, August 29, 2016

VIDEO: Tundu Lissu asema anamkumbuka JK, Mwanasheria mkuu atoa ushauri wa UKUTA

AyoTV kila asubuhi itakua inakuletea uchambuzi wa magazeti ya Tanzania kuhakikisha zote kubwa za siku unazipata, za leo August 30 2016 ziko hapa kwenye hii video.

U

Monday, August 22, 2016

Bashe na Mtazamo Wake Juu ya UKUTA "Jamhuri Inacheza Ngoma ya Chadema"

Bashe na mtazamo wake juu ya #UKUTA
Wanachokifanya hawa UKUTA ni kuitia Serikali hasara. Zaidi ya hilo Chadema wamekuwa PRO ACTIVE na kuwalazimisha "JAMHURI" kuwa REACTIVE. Sasa Jamhuri inacheza ngoma ya Chadema badala ya Chadema kucheza ngoma ya Jamhuri. -
#UKUTA

Sunday, August 21, 2016

Lipumba Aipasua CUF.......Wajumbe Warushiana Viti na Kutukanana, Mkutano Wavunjika


Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ukilenga kuwachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ulivunjika baada ya wajumbe kuanza kurushiana viti na matusi baada ya kupishana katika hoja ya kumtosa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba.

Profesa Lipumba alijiuzulu nafasi yake kabla ya kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka jana akieleza kuwa roho inamsuta kumnadi mgombea urais aliyeungwa mkono na vyama vya Ukawa. Lakini mwaka huu alirejea na kuandika barua akiomba kurejea kwenye nafasi yake hali iliyozua sintofahamu.

Taarifa kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa wajumbe 832 walihudhuria lakini hoja ya kumjadili Profesa Lipumba ilipofikiwa, baadhi ya wajumbe ambao wanamuunga Mwenyekiti huyo wa zamani walizua vurugu wakipinga utaratibu uliotumika.

Baadhi ya wajumbe hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa viongozi waliopo madarakani walifanya ubabe kwa kulazimisha kura ya kukubali au kukataa ombi la Lipumba ipigwe kwa uwazi na sio siri kama Katiba inavyoeleza.

“Haki haikutendeka, ni ubabe. Wala mkutano haikuzingatia kutimia kwa akidi. Tulilazimishwa kupiga kura kwa kunyoosha mikono wakati mazingira yaliyopo na usahihi, kura ni siri,” mmoja wa wajumbe hao alikaririwa.

Baada ya kupiga kura za wazi, Lipumba alipata kura 14 kati ya kura 832 hivyo kuonekana kukataliwa kwa kishindo, lakini vurugu zilizuka ghafla kutokana na maamuzi hayo na mkutano ukashindwa kufanikisha zoezi zima la kuwapata viongozi hao wapya.

Katika hatua nyingine, Juma Haji Duni alijiengeu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo, baada ya baadhi ya wajumbe kusisitiza kuwa katiba inamtaka mtu aliyejiuzulu na kuhamia chama kingine kusubiri miaka miwili ili agombee nafasi ya uongozi ndani ya chama pale atakaporejea.

Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa CUF, Shaweji Mketo, alisema kuwa Duni alijiondoa kutokana na maadui wa Ukawa kutaka kukihujumu chama hicho.

Mkutano huo umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena.

Thursday, August 18, 2016

Salamu ya Maalim Seif yabamba Mitandaoni Nchini

 Picha inayomuonyesha Maalim Seif Sharrif Hamad akiwa ameinama mikono ikiwa tumboni, huku Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akiwa amenyoosha mkono kuashiria kutaka kusalimiana na katibu huyo mkuu wa CUF, sasa imekuwa moto mtandaoni.

Picha hiyo ilichukuliwa wakati wa shughuli za mazishi ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi kisiwani humo mapema wiki hii, na sasa inaigizwa na watu wa kariba tofauti wanaotuma mitandaoni picha inayofanana na tukio hilo.

Picha hizo zinaonyesha watoto, vijana na hata watu wa makamo wakiigiza tukio hilo.

Wawili hao walipambana kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais wa Zanzibar uliofutwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28, siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa mbio za urais. CUF ilisusia uchaguzi mpya uliotangazwa na Jecha.

Vitendo hivyo vya kuigiza matukio ya watu muhimu sasa vimepamba moto mitandaoni. Miongoni mwa matukio yaliyoigwa sana mitandaoni ni la waziri wa zamani wa kilimo, Steven Wasira kupiga picha akiwa hajafunga vizuri vifungo vya koti na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kudondoka.

Pia tukio jingine lililoigwa sana ni la Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuonekana amekaa kwenye kiti pembeni ya barabara akiongea na simu huku msafara wake ukiwa unamsubiri.

Friday, August 5, 2016

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda Apiga Marufuku Maandamano ya UKUTA, Awapa Rungu FFU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwepo kitu kinaitwa UKUTA ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.

Akizungumza na kikosi cha kutuliza ghasia katika kambi ya Ukonga Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa askari wanafahamu sheria wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo au maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshaagiza kinachotakiwa ni utekelezaji.

‘’Msisubiri maelekezo yoyote kutoka juu, asiwepo mtu yeyote atafunga duka kwa sababu ya UKUTA nyie ni matrekta hakuna UKUTA unaweza kusimama mbele yenu, mimi kama Mkuu wa Mkoa ninaamini hatutakuwa na vurugu kwenye Mkoa wetu na hatuwezi kuruhusu vurugu kwa kuwa tunajua madhara ya vurugu’’ Amesema Makonda.

Aidha kwa upande wake Kamanda wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya amesema jeshi la polisi lipo vizuri na vijana wameandaliwa vizuri na wameandaliwa kuwa tayari siku nyingi na hakuna mtu yeyote atakayethubutu kufanya UKUTA na watakaofanya hivyo watazimwa kabla hawajafanya chochote.

Kamada amewataka wananchi wote Jijini Dar es Salaam kuto jitokeza kwenye oparesheni UKUTA kwa kuwa maandamano hayo siyo halali na watakaojitokeza watapata matatizo yasiyowahusu.

Oparesheni UKUTA ilitangazwa na CHADEMA ikiwa na maana Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania na ikatajwa tarehe Mosi Septemba nchi nzima chama hicho kitafanya mikutano ya hadhara jambo ambalo limepingwa na serikali kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufuatia wakuu wa mikoa.

Baba Amwandaa Mtoto Wake Aje Kuwa Raid wa Tanzania 2050, Wasafiri Kwa Baiskeli Kutoka Singida Hadi Dar

Huyu dogo anaitwa Yusuph Mohamed Nassor (2), baba yake Mzee Ahmed Nassor (67) amesema wakati ana mwaka mmoja na nusu alisema anataka kuwa Rais hivyo anamuandaa kuja kuwa Rais wa Tanzania mwaka 2050 kupitia Chama Cha CCM. Yeye na Baba yake wamekuja Dar es Salaam kutoka Singida kwa usafiri wa baiskeli kuja kuonana na Rais Magufuli

Nini maoni yako hapo?

Thursday, July 14, 2016

VIDEO: Sumaye aeleza alivyoshawishiwa kugombea uenyekiti CHADEMA

Leo July 14 2016 Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Frederick Sumaye amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kanda ya Pwani, Sumaye ana wapinzani wawili ambao ni John Gugunita na Gango Kidera, akizungumza baada ya kurejesha Sumaye amesema……
>>>’wanachama mbalimbali na viongozi kutoka kanda hii walifika nyumbani kwangu kama mara tatu na baadae tukakutana sehemu nyingine wakiniomba nigombee nafasi hii na wamenishwishi nimekubali na baadae jana wakasema wao ndio watakaoniletea fomu, nikaijaza na leo nimeirudisha’
Nafasi zingine za uongozi ambazo zipo wazi ni makamu mwenyekiti ambapo watu watatu wamejitokeza kugombea nafasi hiyo akiwemo Saed Kubenea, nafasi ya mwekahazina wagombea watatu wamejitokeza akiwemo aliyekuwa naibu waziri wa kazi na ajira wa serikali ya awamu ya nne, Makongoro Mahanga.


VIDEO: Rais Magufuli amwahidi kazi Meya UKAWA, JKT, Magereza wamkera

AyoTV kila asubuhi itakua inakuletea uchambuzi wa magazeti ya Tanzania kuhakikisha zote kubwa za siku unazipata, za leo July 14 2016 ziko hapa kwenye hii video.

ULIKOSA HII YA POLISI KUHUSU TETEMEKO LA ARDHI DODOMA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Wednesday, July 6, 2016

Magufuli: Walioanza Kulalamika Hakuna Pesa Mifukoni ni Wale Waliozoea Kupata Pesa za Burebure



Haya ni maneno ya mh Magufuli akiwaasa watanzania wafanye kazi kwa badii ili kuweza kujipatia kipato.

Maneno haya ameyatoa alipohudhururia mualiko maalumu kutoka kwa muft mkuu wa dini ya kiislam Tanzania kwenye baraza la la sikuku ya Eid.

Hizi ni salamu kwa wale wote wanaolalamika kwamba

Magufuli: Tusipofanya kazi hatutapata pesa, ndio maana waliokuwa wanapata za kiujanjajanja wanahaha, tushirikiane kuijenga nchi yetu 

Tuesday, July 5, 2016

CUF Yapinga Polisi kushikilia viongozi wao bila kuwashitaki

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimelitaka Jeshi la Polisi kuwapandisha mahakamani viongozi wake wanaowashikilia kwa tuhuma za uchochezi kisiwani Pemba.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa jana, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho, Salim Bimani, alisema kama polisi wana ushahidi wa viongozi wa CUF na wafuasi wao kujihusisha na matukio ya uvunjifu wa amani basi wawapeleke mahakamani.
 
Bimani alisema wanasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kuwaweka ndani viongozi na wafuasi wao kwa muda mrefu bila ya kuwafikisha mahakamani kinyume na haki za binaadamu.
 
“Tunalitaka Jeshi la Polisi kama wana ushahidi juu ya viongozi wetu ambao wanawahusisha na matukio ya uvunjifu wa amani kisiwani Pemba basi wawapeleke mahakamani,” alisema Bimani.
 
Bimani alisema kuwa tokea kuanzishwa mfumo wa vyama vingi Tanzania kumekuwa na unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya raia hasa wanachama wa CUF jambo ambalo alisema kuwa linafanyika kwa nia ya kukikandamiza chama hicho.
 
“Ikiwa sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo kila wakati Zanzibar imekuwa ikishuhudia kuletwa askari wengi katika kipindi cha uchaguzi,”alisema Bimani.
 
Hata hivyo, alisema kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa Oktoba 25, 2015, kumekuwa na hatua kadhaa za unyanyasaji dhidi ya wafuasi wa chama hicho unaofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama.
 
“Haya yote yanayofanyika ili kuzima sauti za watu, lakini tunawaambia viongozi wa CCM pamoja na vyombo vya dola, tutaendeleza msimamo wetu wa haki sawa kwa wote,” alisema Bimani.
 
Alisema CUF inalaani vitendo vya hujuma dhidi ya raia na mali zao unaofanywa kwa lengo la kuvipa sababu vyombo vya ulinzi na hasa wafuasi wake, pamoja na kulaani kauli za vitisho na lugha za kibabe zinazotolewa na Jeshi la Polisi Zanzibar, kama vile iliyotolewa Juni 28 mwaka huu na Naibu Mkurugenzi wa Upepelezi Salum Msangi kisiwani Pemba kwa lengo la kuwanyamazisha wananchi ili kuisambaratisha CUF.

Sunday, July 3, 2016

Tarifa za John Mnyika Kumkataa Lowasa zilizozagaa Mtandaoni Chadema Watoa Kauli...

TAARIFA KWA UMMA

Ipo hoja nyepesi mno iliyopikwa na Vijana wa Lumumba juu ya Mbunge wa Kibamba na Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA John Mnyika kuwa alimkataa Lowassa

Hoja hiyo ni ya kupuuzwa kwa kuwa haina ukweli wowote ule, na nitalishangaa Jeshi la Polisi kuendelea kukaa kimya,na kumuacha aliepotosha Umma kwa kiwango kikubwa kiasi hicho,jambo ambalo limempa Usumbufu mkubwa Naibu Katibu mkuu kwa chama na Wananchi wake katika jimbo lake.

Nataka kuona nguvu ya Cyber Crime kama kweli sheria hiyo ni dhahiri ni msumeno au huwa inakata upande mmoja tu!.Mnyika ni Kiongozi mkubwa na katika Taasisi kubwa sana nchini CHADEMA,hapaswi kunenewa uongo kwa nia ya kuupotosha Umma naliomba jeshi la Polisi liingie kazini Mara moja kutimiza majukumu yake.

Imetolewa July 03

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa

Thursday, June 30, 2016

Wabunge watatu wa Ukawa wasimamishwa kutohudhuria vikao bungeni


Bunge limeridhia pendekezo la adhabu ya kumsimamisha vikao 10 kuanzia leo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kudharau mamlaka ya Spika.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kepten Mstaafu George Mkuchika alisema alinyoosha kidole cha kati kwenda juu cha mkono wa kulia huku vingine akivikunja  jambo ambalo ni matusi na dharau kwa mamlaka ya Bunge.

Naibu Spika Dk Tulia Ackson amewasimamisha Wabunge wengine wawili wa Ukawa,ambao ni Mbunge wa  Ubungo (Chadema) Saed Kubenea kwa kutohudhuria vikao vitano kuanzia leo baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa alisema uongo Bungeni.

Mbunge mwingine  aliyesimamishwa ni  Mbunge wa Simanjiro (Chadema) James Ole Millya kutohudhuria vikao vitano kuanzia leo baada ya kutiwa hatiani na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwa alisema uongo Bungeni.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameanza kutoa hotuba ya kuahirisha Bunge na kueleza bajeti ni ya kihistoria tangu nchi ipate uhuru kwa kutenga asilimia 40 ya Sh29.5 trilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta