Thursday, June 23, 2016

Kijana Akata Uume wake Mkoani Tanga, Adai Aliingiwa na Majini

Kijana mmoja mkoani Tanga Jumatano hii ameziondoa sehemu zake zote za siri kwa kuzikata na kitu chenye ncha kali.

Akiongea katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm Alhamisi hii, Daktari wa Idara ya Upasuaji katika Hospitali ya Muheza mkoani Tanga, Dk. Abas Mussa, amesema jana majira ya mchana walimpokea mgonjwa huyo akiwa hana sehemu zake zote za siri.

“Jana tulimpokea mgonjwa katika chumba kidogo cha upasuaji akiwa ameletwa kwa ajili ya kushonwa,” alisema Dk Abas. Mgonjwa huyo baada ya kumkagua tuligundua kwamba ameondoa sehemu zake za siri, alijieleza kwamba yeye mwenyewe ana tatizo la akili na amehisi kwamba amejiwa na vitu kama mashetani au majini ambayo yalimuamuru kuondoa sehemu zake za siri. Tuliona huyu mtu alitumia kitu chenye ncha kali, mfano wa kisu ambacho aliweza kujiondoa uume wake pamoja na korodani mbili,”

Aliongeza, “Mteja wetu huyu alikuja katika hali ya kumwagika damu, kutokana na jeraha hili kubwa tukaamua kumpeleka katika chumba cha upasuaji, kwa ajili ya kufanyiwa matibabu zaidi, sehemu za siri hazikuwepo kabisa, kwa maana hata ushahidi wa kuziona zikiwa zimebebwa pembini haupo, kwa hiyo itakuwa baada ya kuziondoa zilisalia huko huko ambako aliziondoa, ilibakia sehemu ya wazi ambayo iliweza kushonwa na kurudi kawaida, tulicho jitahidi ni kuhakikisha kwamba hatoki tena damu, lakini pia tumeshona yale majeraha ili aweze kupata uwazi wake wakutoa mkojo, na pia kwa sasa anaendelea vizuri,”

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta