STORI: Imelda Mtema, Wikienda STAA mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu amewafungukia wanaomsema vibaya kuwa siku hizi kafulia mpaka anatembelea usafiri aina ya Bajaj na kudai kuwa hayo ni maisha yake binafsi ambayo hayamhusu mtu yeyote.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Wema alisema kuwa anashangazwa sana na watu ambao wanafuatilia maisha yake kila kona kwa kuwa yeye ni binadamu kama walivyo wengine na maisha yote anastahili kuishi.
“Jamani sijui mijitu mingine ikoje? Bajaj ni usafiri kama usafiri mwingine, sasa cha ajabu nini mimi kuutumia? Mniache na maisha yangu,” alisema Wema.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii