Monday, May 30, 2016

Kidoa Alamba Shavu la Kutangaza Nguo EBM

kidoa
STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA
VIDEO Queen Asha Salum ‘Kidoa’ hivi karibuni ameibua maswali mengi mtandaoni baada ya kutupia picha akiwa ameonesha nguo ya ndani ambapo wengi wamemkejeli kwa picha hizo.
Mwenyewe alipozungumza na Ijumaa Wikienda alisema kuwa, hajali watu wanavyomnanga kwa sababu yupo kimasilahi zaidi kwani amelipwa mkwanja mrefu ambao unakidhi mahitaji yake na anachojua yeye hajaonesha maungo yake bali anafanya matangazo ya nguo aliyoionesha.
“Dah! Najua nimetukanwa sana lakini watambue kuwa mimi ni Balozi wa EBM, kampuni ya nguo, wamenilipa mkwanja mrefu na kila nguo inayotua kwenye mwili wangu ni matangazo sasa siwezi kuwajali binadamu zaidi nikaacha masilahi, kikubwa sivunji sheria,” alisema.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta