Monday, May 30, 2016

Lungi alinanga penzi la Wolper, Harmonize

Harmonizer-na-WolperJacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’
STORI: HAMIDA HASSAN, WIKIENDA
MSANII wa filamu wa kitambo, Lungi Maulanga amelinanga penzi na Jacqueline Wolper na Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ akisema kuwa, anachoona ni kama Wolper anatembea na mdogo wake.
LUNGI (1)Lungi Maulanga
Akiuzungumzia uhusiano wa mastaa hao, Lungi alisema alijisikia vibaya sana kuona shosti wake Wolper kafa, kaoza kwa Harmonize kutokana na tofauti kubwa iliyopo kati yao.
“Unajua Wolper ni kama mdogo wangu na shosti wangu hivyo siwezi kumuacha apotee, mimi nitamuita tutaongea kwa kina, kama atashikilia msimamo wake nitamuacha kwa sababu si unajua mtu akishapenda, lakini kiukweli hawajaendana,” alisema Lungi.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta