Abiria wametakiwa kuondoka kwa dharura kutoka kwenye Ndege ya Shirika la Ryanair iliyokuwa safarini kuelekea Manchester, Uingereza kutokana na tishio la kuwemo bomu.
Ndege hiyo ilikuwa karibu kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Rygge karibu na Mji Mkuu wa Norway, Oslo abiria walipotakiwa kuondoka.
Baadaye ilibainika kwamba hakukuwa na bomu.
Abiria wawili ambao tabia yao ilikuwa imewafanya watu kuwashuku walizuiliwa na polisi kwa muda lakini baadaye wakaachiwa huru.
Taarifa zinasema wasiwasi ulizuka baada ya wanaume hao wawili kusikiza wakijibizana kwa sauti na mmoja wao akataja neno “bomu”.
Polisi wamesema hali ya kawaida imerejea nalo shirika la ndege la Ryanair likasema ndege hiyo itaondoka na abiria karibuni.
Kisa hicho kimetokea saa chache baada ya watu kulazimishwa kuondoka uwanja wa michezo wa Old Trafford, Manchester jana Jumapili baada ya kitu kilichohofiwa kuwa bomu kuonekana.
Baadaye ilibainika kwamba kilikuwa kifaa kilichoachwa na kampuni iliyokuwa ikifanya mazoezi ya kiusalama ikitumia mbwa wa kunusa.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii