Monday, May 16, 2016

Video ya Wema Akidendeka Yamweka Pabaya

Wema
Wema Isaac Sepetu ‘akidendeka’ chumbani na mwanaume.
 Kipande cha video kilichosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii ya Instagram, Facebook na WhatsApp kikimuonesha staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘akidendeka’ chumbani na mwanaume kimemuweka pabaya baada ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo kusema kuwa kama ni sehemu ya filamu haina maadili ya Kitanzania.
wema (1) Akizungumza na Wikienda kwa njia ya simu akiwa nje ya nchi wikiendi iliyopita, Fisoo alisema kuwa kama ni filamu mpya ya mwanadada huyo, ikiingizwa sokoni ikiwa haina maadili yanayotakiwa kamwe hawawezi kuruhusu kusambazwa popote na wala hawawezi kuipitisha.
Kipande hicho cha filamu hiyo kinamuonesha Wema akiwa anadendeka kikwelikweli na jamaa huyo jambo ambalo bodi hiyo imeliangalia kwa upande wa pili na kwamba haitaingia sokoni ikiwa hivyo.
wema (2)Baadhi ya mashabiki wa Wema waliokiona kipande hicho walikuwa na maswali lukuki kichwani kutokana na kile walichokuwa wakikiona kwenye kipande hicho cha filamu hiyo.
“Jamani hata kama ni filamu, hapana, imezidi, kwa kweli ni hatari sana maana kama Wema angekuwa mwanamke wangu hata hiyo filamu angeacha kuicheza kabisa,” alisema mmoja wa mashabiki hao.
wema (3)Kwa upande wake mpenzi wa Wema ambaye ni Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan alisema kuwa na yeye anatamani kupata nafasi ya kucheza filamu, tena apewe vipande kama hivyo hata kama ishirini, atacheza kwa uangalifu.
“Yaani na mimi napenda sana nicheze filamu vipande kama hivyo ishirini hivi tena nitacheza vizuri sana maana najua kila mtu anaweza kuigiza kama hivyo,” alisema Idris.
Kwa upande wake Wema hakutaka kusema chochote juu ya kipande hicho.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta