Stori: Hamida Hassan, Ijumaa
Miezi kadhaa iliyopita liliibuka gumzo kubwa mtandaoni kati ya Timu Wema na Timu Zari kuhusu nani kati ya Wema Sepetu na Zarinah Hassan ‘Zari’ ana wowowo kubwa.
Katika mjadala huo kila upande ulikuwa ukivutia kwake huku mara nyingi Timu Zari wakitumia ile picha aliyopiga Zari na Diamond (Zari kavaa gauni jekundu na Diamond kavaa suti nyeusi) ambapo Timu Wema wao walikuwa wakirusha tu vijembe kuwa, Wema wao hajaladii ila Zari kajaladia kwenye picha hiyo.
Zari na Diamond
Aidha, katika siku za hivi karibuni, Wema aliamua kumjibu Zari kwa kupiga picha iliyo kwenye pozi kama lile la Zari na Diamond huku Wema na jamaa yake huyo aliyedaiwa kuwa ni msanii wakiwa wamevaa nguo kama zile walizovaa Zari na Diamond (angalia picha ukurasa wa kwanza).
Kuanzia hapo ikawa mpambano ni kati ya picha hizo mbili ambazo wadau mbalimbali wamekuwa wakizitupia kwa pamoja.
Hata hivyo, mpaka sasa hakuna upande unaoonekana kuibuka na ushindi hivyo swali la kwamba ni nani kati ya wawili hao ana kalio kubwa jibu halijapatikana.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii