Thursday, May 12, 2016

DIAMOND PLATINUMS KUMMWAGA ZARI THE BOSS LADY,SIRI NZITO YAFICHUKA,MAZITO YASEMWA

Nyuma ya pazia la sakata la staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kutaka kummwaga mama wa mtoto wake, Latifah Nasibu ‘Princess Tiffah’, Zarinah Hassan Tiale ‘Zari The Boss Lady’, kuna siri nzito, Amani limenyetishiwa. 
CHANZO CHAFUNGUKA 
Habari kutoka kwa chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya Diamond zilieleza kuwa, hivi karibuni kuliibuka madai mazito kuwa, Diamond, kama ilivyo tabia yake ya kutodumu na mwanamke kwenye uhusiano wa kimapenzi, tayari ameonesha ishara zote za kuachana na mama Tiffah.

SKENDO YA KUTOKA NA IRENE 
“Ile skendo ya kusemekana Diamond anatoka na Lynn (Video Queen wa Bongo, Irene) kama ingekuwa zamani, ingeweza kuwa tiketi ya wawili hao kumwagana jumla lakini wengi hawajui kuwa si rahisi kiasi hicho kwa siku hizi. Ingawa pia inaaminika, Diamond kuwa na Llyn anaungwa mkono hata na dada yake, Esma.
KUMBE SIRI NI TIFFAH 
“Kwa taarifa yenu, Diamond hawezi kummwaga Zari kirahisi na siri ni moja tu ni Tiffah. Ukweli ni kwamba, Tiffah ndiye anayeshikilia penzi la Diamond na Zari. 
“Unaambiwa Diamond anampenda Tiffah kupita kiasi hivyo hataki kucheza mbali na mwanaye hata kama kuna figisufigisu kati yake na Zari anazivumilia tu. “Hakuna kitu kinachomuumiza Diamond kama malezi ya upande mmoja (ya mama tu) kama ilivyokuwa kwake ambapo alilelewa na mama yake (Sanura Kassim ‘Sandra’) baada ya kutelekezwa na baba yake (Abdul Jumaa). Hivyo hataki mambo kama hayo yamkute Tiffah ndiyo maana hata baada ya Zari kutimkia Sauz (Afrika Kusini) na Tiffah, Diamond amekuwa akimuibukia mara kwa mara kwa ajili ya kuwa karibu na mwanaye. 


“Niamini mimi, kama Zari angekuwa hajazaa na Diamond, mambo yangeshaharibika tangu zamani na wala Diamond asingetumia nguvu kubwa kukanusha kwamba hajaachana na Zari kama alivyofanya juzikati.”
INGEKUWA KAMA WEMA, JOKATE 
“Hivi unajua kwa nini ilikuwa rahisi kumwagana na Wema (Sepetu)? Au Jokate (Mwegelo)? Au Penny (Penniel Mungilwa)? Ni kwa sababu hakuna aliyezaa naye na kama utakumbuka Diamond aliwahi kusema kuwa, ndiyo maana aliachana nao kwa sababu walikataa kumzalia mtoto. Kama kuna ambaye angezaa naye kati yao, hadi kesho wangekuwa pamoja. “Kinachombeba Zari kwa Mond (Diamond) ni kwa sababu ya Tiffah. 
Kwa hapo kweli Zari alicheza kamari na amelamba dume maana jamaa atafanya kila awezalo lakini mwisho wa siku lazima arudi kwa mama Tiffah. “Sisi tunamjua jamaa (Diamond), anapotaka kuachana na mwanamke huwa kunakuwa na figisufigisu kama zile za Lynn. Kunakuwa na madai kisha inafuata habari kamili,” kilifunguka chanzo hicho na kuongeza:

 “Kwa Zari itabidi tu ajifanye hakuna tatizo ili awe karibu na Tiffah ingawa hali si shwari kati yake na Zari. Mwenyewe anasema yupo tayari kufa Kijerumani (na tai shingoni) lakini si kuwa mbali na Tiffah na ndiyo maana kuna baadhi ya ndugu wanadai Zari alitambika, akapata mtoto kwani utu uzima dawa. “Zari alijua kabisa kwamba kumzalia mwanaume ni kati ya mambo yanayoweza kumshikilia asipeperuke kirahisi.”
ZARI VIPI? Mapema wiki hii, Amani lilifika nyumbani kwa mastaa hao, Madale
Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar kumuulizia Zari ambapo kwa mujibu wa mlinzi, tangu mwanamama huyo aondoke na Tiffah yapata wiki mbili zilizopita, hajarejea.

HUYU HAPA DIAMOND
 Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilimtafuta Diamond ambaye alisema yupo nje ya nchi lakini alijibu maswali ya Amani kwa njia ya WhatsApp. Baada ya kusomewa habari zake hizo, Diamond alifunguka kuwa ni kweli anampenda Tiffah kuliko kitu kingine na kwamba ni kweli pia amezidisha na kuongeza mashamsham kwenye penzi lao. “Ni kweli nampenda sana Tiffah na natamani muda wote niwe naye lakini unakuta majukumu yanabana. Tiffah ndiye kila kitu kwangu na ni kweli ameongeza chachu ya mapenzi kati yetu. “Kuhusu Zari, kuna watu wanataka kututenganisha lakini kwa taarifa yao wamechelewa,” alisema Diamond.

MENGI YAMEIBUKA
 Hivi karibuni kuliibuka mambo mengi ikisemekana kwamba, Zari aliamua kuondoka kwa Diamond kufuatia madai ya jamaa huyo kutembea na Irene lakini kama hiyo haitoshi, Zari naye akaonekana akiogelea kwenye bwawa ambalo baadaye mumewe wa zamani, Ivan Ssemwanga naye alitupia picha akiwa kwenye bwawa hilo huko Sauz. Lakini kwa mujibu wa Diamond, yeye na Zari wapo, wanalea mtoto wao maisha yanaendelea. Kuhusu Llyn, Esma yeye aliwahi kuulizwa na kusema anamjua kama ndugu yake kuhusu kuwa na uhusiano na  Diamond hajui lolote na kuhusu mengine hana la kusema! Juzi, mama Diamond hakupatikana kwenye simu kuzungumzia madai hayo baada ya simu yake kuita mara kadhaa lakini bila kupokelewa.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta