VIDEO ambayo inawahusisha baadhi ya wasanii wa Kundi la WCB, akiwemo Harmonize wakimkejeli staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu jana ilichafua hali ya hewa na kuzua sintofahamu mitandaoni. Baadhi ya maneno katika video hiyo yanasema; “Sister duu usitoe mimba kesho ulie kama Sepetu”.
Video yenyewe ipo hapa;
Mashabiki wa Wema walionekana kumsapoti staa huyo na kumponda Harmonize kwa kitendo hicho alichokifanya akiwa na wenzake.
Baada ya sintofahamu hizo, Harmonize aliibuka na kujibu baadhi ya tuhuma hizo akisema video hiyo imevuja bahati mbaya na haijulikani nani kaivujisha. Asema pointi ni nyimbo ya Raymond inayoachiwa leo iitwayo Natafuta Kiki.
Icheck video hiyo hapa;
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii