Wednesday, May 25, 2016

Harmonize: Wolper Bibi? Niacheni Nimempenda Mwenyewe

Wolper-na-Harmonize-(1)Wolper na Harmonize katika mahaba mazito.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ amefunguka kwa wabaya wake wote ambao wanamsema kuwa mpenzi wake, Jacqueline Wolper ni mkubwa kiumri wamuache kwani anampenda hivyohivyo.
Harmonize na Wolper kwa sasa ndiyo ‘kapo’ ambayo ni habari ya mjini kutokana na wawili hao kuwa kwenye mahaba niue ambayo wamekuwa wakionyeshana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Wolper na Harmonize (2)Akizungumza na Mtandao wetu, Harmonize alisema licha ya kushangazwa na maneno hayo ambayo yamekuwa yakisemwa na wabaya wake kuwa Wolper amemzidi umri lakini kwa upande wake amepotezea kwa madai kuwa mapenzi hayaangalii umri.
“Nashangazwa na watu ambao wamekuwa wakinisema kuwa Wolper ni kama bibi kwangu maana amenizidi kiumri lakini wanashindwa kutambua kuwa mapenzi huwa hayaangalii masuala hayo, sasa mimi nawaambia waniache kwani nimempenda mwenyewe,” alisema Harmonize.
CHEKI VIDEO: WOLPER NA HARMONIZE WAKIJIACHIA KIMAHABA

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta