Wednesday, May 25, 2016

Isabela Aachwa… Karama Aoa Kifaa Kingine

KALAMA (2)
DAR ES SALAAM: Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, aliyewahi kutamba na Kundi la Gangwe Mob, Luteni Karama ambaye kwa muda mrefu anafahamika kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Isabela Mpanda, Jumamosi iliyopita alimuacha kwenye mataa na kufunga ndoa na mrembo Aisha Yassin, Mkazi wa Magomeni Mikumi jijini Dar.
ISABELA.pngIsabela
Shughuli hiyo ilianza mapema, lakini ilipotimu saa tisa jioni, umati ulikusanyika nyumbani kwa mrembo huyo kumshuhudia nyota huyo wa Bongo Fleva akikabidhiwa ‘kifaa’ hicho ili kuanza maisha mapya ya ndoa.
KALAMA (4)Ikionekana kama ni jambo la siri, hakukuwa na staa yeyote wa Bongo Fleva aliyeshuhudia tukio hilo jema, zaidi ya mpambe wa bwana harusi na ndugu wa familia zote mbili.
KALAMA (5)Wakati wote wa shughuli hiyo, ndugu wa kike wa mwanaume walikuwa wakiimba nyimbo za kuwasifu maharusi hao, kabla ya waalikwa kupata chakula kilicho-letwa rasmi kutoka mahali kusiko-julikana.
KALAMA (3)Kufuatia tukio hilo, paparazi wetu alimtafuta mpenzi wa muda mrefu wa mwanamuziki huyo, Isabela ambaye alipoelezwa kuhusu tukio hilo, alisema hana taarifa zozote ingawa hata hivyo, alishaachana na Mbongo Fleva huyo kiasi cha miezi mitatu iliyopita.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta