BAADA ya kuripotiwa kuwa mwanamuziki, Baby Madaha ‘amezama’ kimapenzi kwa mchumba wake aliyekuwa akiishi naye Dubai, sasa msanii huyo amekwenda mbali zaidi na kuamua kufanya
biashara za kimuziki akiwa nchini humo.
Baby ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu katika masuala ya muziki, hatimaye ameeleza kwamba ana mpango wa kuachia muvi hivi karibuni lakini hajaitaja jina pamoja na video ya muziki wake mpya alioifanyia nchini Dubai na jijini Dar es Salaam inayoitwa Corazon.
“Nimeamua kufanya video ya wimbo wangu mpya huku Dubai kutokana na kuwepo huku mara kwa mara lakini pia kuna vipande vimefanyika Dar es Salaam. Hiyo itakuwa ndiyo ngoma yangu mpya ya kurejea kwenye game inaitwa Corazon maana yake Moyo, sijamshirikisha mtu kwa sababu nimepanga kurejea mwenyewe kwanza,” alisema Baby
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii