DAR ES SALAAM: Miezi michache tu baada ya staa wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuripotiwa kutoka na msichana anayejulikana kama Chaga Baby, imedaiwa kuwa hivi sasa, yupo na mrembo raia wa Ethiopia (Mhabeshi) anayejulikana kwa jina la Addi na ameapa kufunga naye ndoa.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa, Nay na mwanadada huyo ambaye ni msanii wa filamu, kwa sasa ni mahaba niue na wanapoelekea ni pazuri tofauti na wapenzi wengine waliopita, kwani huyu humzungumzia kila wakati.
Nay alitafutwa na alipopatikana alikiri kuwa na uhusiano na raia huyo wa Ethiopia, huku akikazia kuwa baada ya kurukaruka sana ana mpango wa kumuoa kabisa.
“Nimesharukaruka vya kutosha, sasa nimetulia na mchumba wangu huyu Addi tuliyekutana uwanja wa ndege huko Afrika Kusini wakati nikiwa narudi Bongo na yeye anarudi kwao, tangu hapo tulianza uhusiano na tunae-ndelea vizuri.
“Sija-wahi kusema kuhusu kuoa, lakini kwa huyu ndiye mke wangu ajaye maana tulipofikia ni pazuri, anawapenda sana watoto wangu, sitaki Wabongo wamzoee maana wataniharibia na maneno yao,” alisema.
Staili ya kukutana kwa wapenzi hao, inafanana na ilivyokuwa kwa Diamond na Zari, ambao pia walikutana ndani ya ndege nchini humo, lakini wenyewe wakiwa na uelekeo mmoja wa Dar es Salaam.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii