May 25 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, vilabu vya Yanga na Azam FC vilikutana kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC), katika mchezo huo Azam FC ilifungwa magoli 3-1, magoli ya Yanga yakifungwa na Amissi Tambwe dakika ya 9 na 47 huku Deus Kaseke akipachika goli la mwisho, , Azam FCwalipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Kavumbagu.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii