Tuesday, August 9, 2016

Linah aeleza kwanini watu wanahisi anatoka kimapenzi na Billnas

Msanii wa muziki, Linah Sanga amekanusha tetesi ambazo zilisambaa katika mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na rapper Billnas.
linnah

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Raha Jipe Mwenyewe’ hivi karibuni, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa Billnas ni mshkaji wake.

“Watu wanatakiwa wajue tu kuwa mimi na BillNas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu sana,” alisema Linah “Saizi mimi na Bill Nas ni washikaji sana maana siri yake ndiyo siri yangu,”

Aliongeza, “Bill Nas ndiye aliyenishauri nibadilike kwenye muziki na kunipa ‘connection’ na ‘Producer’ T Touch, yeye ndiye aliniambia nibadili mfumo mzima wa muziki wangu na ndiyo nikafanya hivyo,”

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta