‘Zigo Remix’ ya AY bila shaka ndio wimbo ambao umevunja rekodi ya hits za mwimbaji huyo kwa kupenya hadi kwenye masikio ya wanasiasa wakubwa Afrika Mashariki licha ya kuwa na ujumbe wa kumsifia mrembo, wajaluo wanaita ‘atoti’.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ameonesha alivyo mmoja kati ya mashabiki wakubwa wa wimbo huo baada ya kuutumia kama ‘dedication’ kwa watu ambao hawakuwa kwenye mkutano wake na kisha kuutendea haki akisindikizwa na wasaidizi wake.
“For those who are not here, who are… wherever you’re. That’s what we call ‘kula kwa macho’,” alisema Odinga kabla hajashusha kikuza sauti na kuanza kuitikia wito wa DJ ambaye alionekana kuwa alimpanga awali kuachia kipande cha wimbo huo kinachosema ‘nakula kwa macho’.
Zigo Remix ya AY aliyomshirikisha Diamond Platinumz, imepikwa na watayarishaji wakubwa watatu, Nahreel, Hermy B na Marco Chali hivi sasa video yake imefikisha views zaidi ya milioni 6 tangu ilipowekwa mtandaoni Januari mwaka huu
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii