Wednesday, May 25, 2016

Wanaogoma kuuza ‘condom’ kukiona!

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Abdul Shaweji
Wafanya-biashara wa Famasi na bidhaa za kawaida wanaosonya, kutukana, kutema mate na kukataa kuuza kinga ya mipira ya kiume (kondom) kwenye maduka yao ili kuiokoa jamii na maambukizi ya magonjwa ya ngono kama Ukimwi na kuzuia mimba zisizotarajiwa, wametakiwa kuacha mara moja na kwamba atakayekiuka lazima atakiona.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Afisa Mauzo wa Shirika la PSI-Tanzania mkoani Njombe na Ruvuma, Kinyumbi Kinyumbi wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wadau na wasambazaji, wauzaji wa kondom iliyofanyika kwenye Ukumbi wa VETA Manispaa ya Songea.
Kinyumbi alisema kuwa, baadhi ya wafanyabiashara bado hawajajua umuhimu wa kondom kama bidhaa inayotakiwa kuwekwa na kuuzwa sehemu zao za biashara kutokana na imani za kidini na mitazamo hasi.
“Bado jamii haielewi vizuri kuwa kondom ni bidhaa ya afya inayowakinga na magonjwa ya ngono kama Ukimwi na mengine ya zinaa pamoja na uzazi wa mpango kama ikitumika sawasawa na kwamba ni sawa na bidhaa nyingine kama chumvi na sukari hivyo kukataa kuuza ni kosa kisheria.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa PSI mkoani hapa na Njombe, Wilfred Mkungilwa alifafanua kuwa, PSI kama mdau katika usambazaji wa kondom ina lengo la kuikinga jamii dhidi ya hatari ya maambukizi mapya ya Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa.
Naye Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Abdul Shaweji aliwataka wafanyabiashara kuchangia juhudi za serikali za kuhakikisha bidhaa bora za afya zinapatikana kwa urahisi na kwa wakati.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta