Wednesday, May 11, 2016

Nimemuweka Wazi Mpenzi Kupunguza Usumbufu - Ommy Dimpoz

Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake 'Achia boy' amefunguka na kusema kuwa ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ili kupunguza usumbufu kutoka kwa watoto wa kike.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio, Ommy Dimpoz alidai kuwa kufanya hivyo ni kupunguza kasi ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakimsumbua na kumtaka kimapenzi.

"Unajua saizi nimeamua kumuweka wazi mpenzi wangu ili wajue yupo na kupunguza usumbufu kwa watoto wa kike ambao wanadhani labda niko single, japo yupo mbali lakini kufanya hivyo inasaidia" alisema Ommy Dimpoz

Mbali na hilo Ommy Dimpoz alisema mpenzi wake huyo kwa sasa anasomea udaktari nchini uingereza na kudai ni mtu wa Afrika Mashariki.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta