Wednesday, May 11, 2016

Diamond Atoa Sababu ya Kutosema Chochote wakati Anashoot Video na P-Square ‘Video Ninayo Tayari’ (Video)


Diamond Platnumz aliamua kutosema chochote wakati alipokuwa Afrika Kusini kufanya video ya wimbo aliowashirikisha P-Square. Ni Paul na Peter Okoye tu ndio waliopost picha za behind the scenes za uchukuaji wa video hiyo.

“Sometimes naonaga ukianza kuelezea kitu kitakuja, kitakuja, kinakuwa kinaboa,” Diamond ameiambia Bongo5.

“Sema tumeshamaliza tumeshashoot video, nasubiria tu mimi mwenyewe, nimekaa nayo tu ndani naangalia nitoe saa ngapi, imeshaisha kila kitu. Na muziki sometimes unafaa kuchungulia kuangalia unaiweka wapi, na kwasababu sio kutoa tu nyimbo unataka uonekana umefanya wimbo, lakini pia unatoa nyimbo kwa target za kibiashara,” ameongeza.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta