Polisi Kanda maalum Dar es salaam kupitia kitengo cha usalama barabarani wametoa taarifa ya makosa ya barabarani kuanzia May 20 2016 hadi May 29 2016 kuwa wamekamata magari mbalimbali kwa makosa ya usalama barabarani na jumla ya Tsh Milioni 548.16 zimekusanywa ikiwa ni faini kwa makosa hayo kwa muda wa siku 9.
Aidha Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro alitoa taarifa ya kukamatwa kwa mume wa Mtumishi wa wizara ya fedha Aneth Msuya ambaye ni mdogo wa Bilionea Erasto Msuya.
Marehemu Aneth Msuya aliuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake eneo la kigamboni Dar es salaam pia wanaendelea kumtafuata dada wa kazi ambaye aliacha kazi siku moja kabla ya mauaji kutokea.
UL
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii