Moja kati ya stori zinazogonga vichwa vya habari vya magazeti ya michezo Tanzania ni kuhusiana na wazo la mfanyabishara na mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kuomba kuikodi Yanga katika kipindi cha miaka 10, hili ni wazo ambalo kila mmoja ana mtazamo wake, Ayo TV imempata mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe azungumzie mtazamo wake kuhusiana na wazo la Manji.
“Kukodi Yanga hili ni suala gumu sana kuliko hata la Simba na linahitaji elimu kubwa zaidi bora la Simba ni suala ambalo watu tunauelewa nalo kuliko la Yanga, ila hili la Manji sijawahi kuona kwa sababu Manji anataka kuchukua timu ya wakubwa na logo ya Yanga ila mashabiki wanashangilia na hawajiulizi timu yao ya vijana itakuwaje”
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii