Tuesday, August 9, 2016

MUWASHO MWILINI UNAMAANA GANI KINYOTA

Mara nyingi mtu huhisi muwasho hasa mkononi unyayoni gotini,tumbon,matakon n.k.
katika nyota tunaamini kila kitu kinamaana
Muwasho unatabiri jambo flani.

Kama hivi:~
Ukiwashwa kwenye:~

  • ~Kiganga cha kulia au kifundo cha mguu wa kulia utapata pesa,
  • ~kiganja cha kushoto na kifundo cha mguu wa shoto utapoteza pesa,
  • ~ukiwashwa tumboni utapewa mualiko au utaalikwa kwenye sherehe au tafrija,
  • ~ukiwashwa makalioni utapata suluhu ya jambo lako,au utatatuliwa shda zako au utateuliwa kuwa msuluhishi,
  • ~gotini utapata khabari za umbeya,uongo,
  • ~ukiwashwa pajani utahama kutoka ulipo kwenda pengne,utahamishwa,
  • ~jicho likicheza kama la kulia utapata furaha,tafrija,mambo mazuri na mwanga,
  • ~kushoto itakuwa kinyume na jicho la kulia,
  • ~puani nje ya ngozi utapata kero,
  • ~kifundo cha mguu wa kulia utalipwa madeni yako au utapata pesa,
  • ~kushoto utadaiwa,au wanaokudai watakuja.
  • ~ukiwashwa kichwa utapata pesa kiurahisi,biashara za harakaharaka

Napenda ya makalio na kichwa
Wewe je?

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta