Dhana iliyojengeka kichwani mwa wakaka wengi ni kwamba wanawake wana mambo mengi sana na wanahitaji mambo mengi sana ili waweze kupenda,dhana hiyo siyo ya kweli.
Kuna njia mbalimbali za kumfanya msichana avutiwe na wewe na nimeviweka hivyo vitu hapo chini basi soma kwa uangalifu na uchukue hatua nzuri zitakazo kusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.
1.WAKAKA WANAOPENDA WATOTO.
Wasichana wanapenda sana wakaka wanaopenda watoto kwa kiasi kikubwa na wanaowafanya watoto wafurahie kuwa na wewe.Inasemekana kuwa wakaka wanaopenda watoto wanasadikika kuwa watakuwa ni baba bora.
2.WAKAKA WANAOJUA KUCHEZA MZIKI VIZURI.
Unaweza ukawa hujui hili lakini ujue sasa kwamba wasichana huwa wanapenda sana wakaka ambao wanajua kucheza mziki basi fanyia mazoezi swala hili utaona matokeo mazuri
3WAKAKA WACHESHI.
Wakaka wacheshi hupendwa sana na wasichana kwa kiasi kikubwa sana,hii ni kwa sababu wasichana hupenda sana wakaka wanaoweza kuwafanya wacheke na kufurahi wanapokuwa karibu nao.
4.MKAKA ANAYE JUA KUVAA VIZURI.
Wasichana wanapenda sana wakaka ambao wanapenda kutokelezea kwa kiswahili cha mjini tunasema kuwa,wakaka wanaopenda kunyuka pamba vizuri.Kama inavyosemekana muonekano wako wa kuvaa ni kadi yako ya kufanyia biashara.Ndio maana ni nadra sana ukamkuta mkaka akavaa vizuri akamtongoza msichana na yule msichana akakataa.
5.MKAKA ANAYEJUA KUPIKA VIZURI.
Wakaka wengi wanajua kuwa kazi ya kupika ni kazi ya wasichana,kwa taarifa yako jifunze kupika chakula,itakushangaza kuona kuwa wasichana wanapenda sana wakaka ambao wanapika chakula kizuri.Kitendo hiki huwavutia sana wadada.
6.MKAKA ANAYE NUKIA VIZURI.
Kwa taarifa yako wasichana wanapenda sana wakaka wanaonukia vizuri,kwa sababu hicho ni kitu cha kwanza ambacho msichana anagundua uwepo wapo
7.WAKAKA WACHAPAKAZI.
Wakaka wanaojishugulisha na kazi ndogo ndogo,wakaka wanajua kufanya mambo madogo madogo kama kufunga bomba,kutengeneza simu yake au laptop yake.au kutengeneza mlango ulioharibika na mambombalimbali ambayo yanahitaji uwepo wako.Wasichana wanapenda sana wakaka ambao wanageuka na kuwa Tool box.
8.MKAKA MWENYE MALENGO.
Hakuna kitu ambacho kinachowavutia wasichana wengi kama mkaka ambaye anamalengo mbalimbali
Wakaka wengi wanafikiri kuwa wasichana wengi wanapenda wakaka ambao ni matajiri,lakini ukweli ni huu ukiwa na malengo mazuri katika maisha ni swala tosha sana kwa kupendwa na msichana yoyote yule,Hata kama hujaumbwa kufanya biashara na huwezi kufanya biashara jitahidi kubuni vitu vya kimaendeleo.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii