MWANDISHI WETU, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Ushoga? Mzungu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja lakini akijitambulisha kuwa ni raia kutoka nchini Italia, hivi karibuni alinaswa akiwa katika harakati za kulawitiwa na vijana watatu, Wikienda limeinyaka.
Tukio hilo lililotafsiriwa kuwa linakwenda kinyume na msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu sheria za makosa ya kujamiina, lilijiri Agosti 4, mwaka huu, nyumbani kwa Mzungu huyo, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
YALIANZA MALALAMIKO
Awali, kijana mmoja alipiga simu kwenye ofisi za Global Publishers na kutaka msaada kutoka kwa kitengo maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kusema kuwa kuna Mzungu amekuwa akimtaka awapeleke vijana nyumbani kwake kwa ajili ya mambo yasiyopendwa na watu wengi na pia ni kinyume na msimamo wa serikali. Lakini atatoa mshiko wa nguvu.
Baada kudakwa na polisi, kupigwa pingu na kupelekwa kituoni.
“Jamani kuna Mzungu anatushangaza kidogo. Ameniambia niwatafute vijana pamoja na mimi mwenyewe twende nyumbanai kwake. Anasema anataka mapenzi yale yanayokemewa na serikali yetu ya Tanzania, mimi nahisi anatakiwa kukomeshwa kama ni tabia yake,” alisema mtoa habari huyo.
BAADA YA TAARIFA
Kufuatia madai hayo, Wikienda lilijipanga kufanya uchunguzi kupitia OFM lengo likiwa ni kujiridhisha kuhusu maneno ya mtoa habari huyo.
Lilikutana na kijana huyo (jina tunalo) ambapo walitafutwa vijana wengine wawili akiwemo OFM mmoja, jumla wakawa watatu na kumkubalia Mzungu huyo.
Katika mazungumzo yake na Mzungu huyo, kijana huyo ambaye ndiye kinara na wenzake waliahidiwa kupewa shilingi laki moja (100,000) kila mmoja kama malipo ya shughuli hiyo ambayo wao haikuwa kwenye ratiba ya siku.
OFM POLISI
Ili kukamilisha uchunguzi wake, OFM ilitinga Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar ili kutoa taarifa za madai ya uwepo wa Mzungu huyo na ‘michezo’ ambayo anadaiwa kuifanya Bongo.
Baada ya kujieleza kituoni hapo, askari wa kituo hicho walitoa ushirikiano mkubwa kwa kufungua jalada lenye namba KJN\ RB\8514\16 TAARIFA na kumtaka kijana huyo kutoa ushirikiano kwa OFM.
ENEO LA TUKIO
Baada ya hapo, safari ya kwenda nyumbani kwa Mzungu huyo ilianza huku kijana huyo akiwa anawasiliana naye kwa taarifa kuwa, wapo njiani.
MAZINGIRA YA NYUMBA
Ugumu ulikuwepo kwenye kuingia ndani ya nyumba hiyo kwani, ilizungukwa na fensi ya ukuta wa matofali, akiishi peke yake. Mzungu huyo aliwaingiza vijana hao watatu waliokusudiwa huku OFM wengine na askari polisi mmoja wakijibanza sehemu kusubiri.
NDANI YA CHUMBA
Baada ya kuingia chumbani, OFM alianza kupiga picha kwa siri, aliweza kumfotoa Mzungu huyo akiwa na wenzake katika mapozi mbalimbali.
Hata hivyo, OFM aligoma kushiriki tukio hilo jambo linalodaiwa kumkera mtuhumiwa huyo na kuamua kuwafukuza wote ndipo songombingo kubwa ilizuka ambapo Mzungu huyo aliwataka waondoke wote.
Akiwa anawatoa nje, ndipo OFM wa nje na askari mmoja walimnasa Mzungu huyo kwa mapicha na kumfunga pingu ambapo kazi ya kumpeleka kituoni ilikuwa chini ya polisi huyo. Wikienda linaendelea kufuatilia ili kujua kilichoendelea.
MAKONDA APONGEZWA
Hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa kauli ya kupambana na watu wanaojihusisha na vitendo vya ushoga akisema ni kinyume na msimamo wa serikali.
Wakati wa kumkamata Mzungu huyo, baadhi ya watu waliokuwa kwenye nyumba za jirani walimpongeza Makonda kwa tamko lake hilo wakisema lililenga kuiweka jamii ya Dar es Salaam katika maadili ya Kimungu.
“Jamani huyo Mzungu aende tu. Juzijuzi Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda alitoa tamko la kupinga ushoga, si jadi yetu jamani! Makonda aliliona hilo ndiyo maana Mungu alimtumia aseme vile, tunampongeza ila mwambieni alifanyie kazi na hili,” alisema mkazi mmoja bila kutaja jina lake.
Juzi, Wikienda lilimpigia simu Makonda kwa lengo la kumpongeza kwa kauli yake hiyo lakini pia kumjulisha hili la Mzungu lakini simu yake mara zote ilikatwa hali iliyoashiria kuwa, alikuwa kwenye kikao au tukio ambalo asingeweza kuongea.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii