Mwanamke kutoka Kenya alitembezwa kwenye mitaa ya Daresalaam baada ya kukamatwa akiiba begi la mkononi(Mkoba )alipokuwa ameenda hapo Mlimani city.
Mashahidi wanadai kuwa,haikuwa ni mara yake ya kwanza kwani amekwisha iba begi lingine katika wiki iliyopita.
Video hiyo ilipostiwa siku ya jumatano Julai 13 kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanamke akilazimishwa kutembea kwenye mitaa ya jiji la Dar les alaam akibeba bango la kujitambulisha kwamba alikuwa mwizi
“Mimi ni mwizi kutoka Kenya ” Ndivo lilivyo someka bango hilo.
Mwanamke huyo inasemekana kuwa haikuwa mara yake ya kwanza kuiba mkoba katika Jumba hilo ndio maana wakaamua kuweka mtego wa kumnasa kilaini kabisa.
TAZAMA VIDEO HIYO HAPA CHINI LIVE NIMEKUWEKEA KAMA BADO HUJAISOMA
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii