Tuesday, July 5, 2016

Nay wa Mitego Awataka Wasanii Kuiga Mfano wake

MSANII wa Hip Hop mwenye ‘title’ kubwa Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema kuwa wasanii wanaofanya gemu la Muziki wa Hip Hop nchini hawana budi kuiga ‘system’ ya jinsi anavyofanya kazi ili kuweza kufikia malengo yao hata kuwa wasanii wakubwa, wenye heshima na mtaji wa mashabi lukuki.

Akichonga na Uwazi Showbiz, Nay anayetamba na ngoma ya Saka Hela kwa sasa alisema watu wanaomfuatilia wataona kuwa amekuwa na utaratibu mzuri hasa wa kutoa kazi kwa kuangalia soko linataka nini na yeye afanye nini jambo ambalo linamfanya awe juu kipindi chote.

“Unajua wasanii wengi wanashindwa kufikia malengo yao kwa sababu hawafahamu namna ya kucheza na mashabiki, mimi ninawataka wanifuatilie na kuiga mfano wangu waone kama hawatafanikiwa kufika wanapotaka,” alisema Nay.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta