Thursday, June 23, 2016

Wakonta: Msichana aliyegongwa gari kwenye mahafali yake ya kidato cha 6 na kupooza mwili mzima ana mkasa utakaokutoa machozi

likuwa ni siku ya furaha ambayo kila mwanafunzi wa kidato cha sita huwa nayo katika nyakati kama hizo. Nyakati ambazo wanafunzi huijiwa na matumaini ya kuyasogelea maisha ya chuo kikuu na kuutua mzigo mzito waliouhangaika kwa miaka miwili migumu ya kukesha kujisomea kutengeneza kesho yao. 

Wakonta (wa kwanza kushoto) akiwa na wenzake siku ya mahafali
Siku ya mahafali ya kumaliza kidato cha sita hujawa na bashasha, hisia za ushindi, dalili za mafanikio, tabasamu halisi, vicheko vya kina na wakati mwingine vikiambatana na machozi ya furaha. 
Wakonta Mapunda, alikuwa mmoja wa wasichana wa shule ya sekondari ya wasichana ya Korogwe, mkoani Tanga waliokuwa na furaha tele kwenye mahafali ya kidato cha sita miaka minne  iliyopita.
Hiyo ilikuwa ni siku iliyoanza kwa furaha kubwa, na kumalizika kwa huzuni kuu. Ilikuwa ni siku iliyobadilisha maisha yake na kuthibitisha ule usemi ‘hujafa hujaumbika.’ Ilikuwa ni siku iliyozima ndoto zake.
“Wiki moja kabla sijafanya mtihani wangu wa mwisho siku ya mahafali mwaka 2012 Februari tukiwa tunajianda kwa mahafali,mmoja wa mwanafunzi mwenzetu aliwasha gari na kuweka reverse kwa kasi sana hivyo kunigonga pamoja na baadhi ya wanafunzi,” ameandika Wakonta kwenye mtandao wa Instagram kusimulia kisa chake.
“Hapo ndio ilipokua mwanzo wa safari yangu ambayo sijawahi hata kuifikiria kwani nilivunjika uti wa mgongo na kupooza kutoka mabegani mpaka miguuni. Nilifanyiwa operation Muhimbili bila mafanikio.Nimekuwa mtu wa kukaa na kulala tu,” aliongeza. Post yake imevuta hisia za watu wengi na kupata comments zaidi ya 400.
image
Wakonta akiwa amelazwa Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji
Akiwa hawezi kufanya lolote kwakuwa mwili wake wote umepooza, Wakonta alilazimika kuishi kwa kutumia alivyobakiwa navyo. Hakutaka kuendelea kuhuzika kwa ajali iliyotokea na kuyakatia tamaa maisha. Hakutaka kipaji chake cha uandishi kife lakini kwakuwa mikono yake haifanyi kazi tena, angewezaje kuandika? Aliufundisha ulimi wake kufanya kazi hiyo.
image
“Mwaka huu 2016 lilitokea shindano la kuandika movie lililodhaminiwa na MAISHA FILM LAB ya Uganda,” aliendelea.
image
“Kwa kutumia ulimi niliweza kuandika na kufanikiwa kuchaguliwa hatua ya kwanza ya mashindano.Hivyo kuhitajika kufika Zanzibar tarehe 6 na kukaa huko siku 10.”
image
Akitoka kwenye familia ya kawaida iliyopo mkoani Rukwa, Wakonta ana nia ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo lakini uwezo hana na anahitaji msaada kutoka kwa Watanzania wenzake.
“Kutoka kijijini kwetu hadi Zanzibar ni km2620 kwenda na kurudi, gharama ni milioni 4 ambazo siwezi kuzikimu. Nahitaji msaada wa hali na mali ndugu zangu ili kuweza kukuza kipaji changu. Mawasiliano na mchango,  0683886446 Airtel money,+255 755 836 896,M pesa.”
image
Nawe pia unaweza kuwa mmoja wa watu watakaomwezesha Wakonta kutumiza ndoto yake. Toa chochote ulichonacho kwa kutumia namba hizo juu.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta