Wednesday, June 1, 2016

Sokwe aliyemburuta mtoto azua zogo

Washington, Marekani. Mauaji ya Sokwe katika mbuga ya wanyama ya Cincinnati nchini Marekani yamezua utata katika mtandao wa Twitter huku kukiripotiwa pia kuibuka kwa malumbano makali baina ya baadhi ya watetezi wa wanyama na makundi ya kiharakati.

Sokwe huyo anadaiwa kumuangusha na kumburuta kijana wa kiume mwenye umri wa miaka minne.

Sokwe huyo alipigwa risasi na kuuawa kufuatia kisa hicho cha kumburuta mtoto.

Watu katika mtandao wamesema sokwe huyo aliyetambulika kwa jina la Harambe hangestahili kuuawa kwani hakuwa na nia ya kumdhuru mtoto huyo.

Huku wengine wakisema wazazi wa kijana huyo ndiyo wa kulaumiwa kwa kukosa kumuangalia mtoto wao.

“Tunaona kulikuwa hakuna sababu zozote za kuuawa kwa soko huyo kwa vile hakuwa na nia yoyote mbaya,” yalisomeka baadhi ya maneno kwenye mitandao hiyo iliyokuwa ikijadili tukio la kuuawa kwa sokwe huyo.

Baadhi ya wachangiaji kwenye mitando hiyo walienda mbali zaidi kwa kuwatuhumu wazazi kwa mtoto huyo na kusema kuwa wao ndiyo sababu ya kuawa kwa sokwe huyo.

“Kwa kiasi watu wa kulaumiwa ni wazazi wa mtoto huyo kwa vile walishindwa kuwajibika,” alisema mmoja wa wachangiaji kwenye mitandao ya kijamii.

Maofisa wa shirika la wanyama pori walisema walichukua hatua hiyo dhidi ya sokwe huyo baada ya maisha ya mtoto huyo kuwa hatarini.

Zaidi ya watu 60,000 wametia saini malalamiko hayo ya kipekee wakitaka wazazi wa kijana huyo kuchuliwa hatua kwa kukosa kumlinda mtoto wao na uzembe uliosababisha kifo cha sokwe.

Juzi, wafanyakazi wa hifadhi moja ya wanyama nchini Marekani walimpiga risasi na kumuua sokwe mmoja baada ya mtoto mmoja kuingia kwenye hifadhi hiyo.

Mkurugenzi wa hifadhi ya Cincinnati alisema mtoto huyo alitambaa na kupita kizuizi kisha kuangukia mahali alikokuwa sokwe huyo ambaye alimshika na kuanza kumburuta.

Aliitaja hatua ya kumuua sokwe huyo kama uamuzi mgumu lakini ulio muhimu.

Mtoto huyo hakupata majeraha mabaya na anaendelea kuangaliwa na wazazi wake.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta