shamsaAkizungumzia nguo anazopenda kuvaa, mdada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Terry alisema, kuna mtu huwa anampelekea nguo ‘classic’ za mitumba na anachagua zile zinazomfaa, ananunua na kuzivaa.
“Niseme tu ukweli kwamba, napenda sana nguo za mtumba, hata makufuli. Huwa nanunua, nazifua na kuziweka ‘sopusopu’ kisha navaa, sioni shida katika hilo,” alisema Shamsa.
Serikali iliwahi kupiga marufuku uuzwaji wa nguo za mitumba za ndani kama vile makufuli, brazia na soksi lakini bado nguo hizo zimekuwa ni kimbilio kwa watu wengi wakidai zina ubora na ni za kijanja zaidi.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii