Akiongea kwenye eNews ya East Africa TV, Baraka amesema hajwahi kufanya kitendo kama hicho kwani walikuwa sehemu yenye watu wengi, na pia hajawahi kuwaza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linah.
“Siwezi kufanya kitu kama hicho kwa sababu pale pana watu wengi, ile picha ilikuwa ya kawaida, yule aliyeipiga na kuipost amekuwa kama kaikuza, sijawahi kufikiria hata kutoka naye”, alisema Baraka.
Pia Baraka amesema siku ya tukio ambayo ilikuwa ni siku ya kuadhimisha miaka 10 ya muziki wa Christian Bella, aliondoka mapema na hakufanya tukio lolote baya.
“Nimetoka kuperfom nikaondoka zangu, sikukaa hata nusu saa, nimemaliza nikaondoka, wasiwe wanaamini mambo ya hivyo”, alisema Baraka.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii