Thursday, May 26, 2016

Wanafunzi Ambao 'Hawakufuzu' Kufukuzwa Vyuoni Tanzania


Maelfu ya wanafunzi wa vyuo na vyuo kikuu nchini Tanzania wako hatarini kufukuzwa katika vyuo hivyo baada ya mamlaka kugundua kashfa kubwa inayohusisha usajili wa wanafunzi ambao hawakufuzu.

Waziri wa elimu Joyce Ndalikacho ametangaza kuvunjwa kwa bodi ya tume ya vyuo vikuu nchini humo na kuwasimamisha kazi kwa mda maafisa kadhaa waandamizi.

Magazeti ya the Guradian na Citizen nchini humo yanasema kuwa serikali imewafukuza wanafunzi 489 ambao walikuwa wamesajiliwa katika chuo kikuu cha St Joseph na kupewa mikopo ya serikali licha ya kuwa hawakufuzu kusomea ualimu.

Serikali imefunga chuo hicho kikuu kazkazini na kusini mwa Tanzania.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta