Ligi kuu soka Tanzania bara wote tunajua imemalizika, baadhi ya vilabu vimeshaanza kufanya usajili kama Yanga tayari wamemsajili Hassan Kessy wa Simba na Juma Mahadhi kutoka Coastal Union ya Tanga.
Wakati tunajiuliza Juma Kaseja atacheza klabu gani msimu ujao baada ya kumaliza mkataba na Mbeya City, mtu wangu wangu Juma Kaseja kaeleza washambuliaji wake hatari katika msimu wa 2015/2016, yaani hao ndio wachezaji wanaoweza kubadili matokeo muda wowote.
“Mimi naweza kusema watanzani huwa hatuukubali ukweli ila tumekuwa tukiuamini uongo, lakini mimi nimekuwa muumini wa kuukubali ukweli, mimi katika washambuliaji hatari msimu huu uliyomalizika ni Tambwe, Kiiza, Kipre, Bocco na Ngoma yaani hao wanaweza kubadili matokeo muda wowote”
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii