Kadri Teknolojia inavyozidi kukua kila siku katika upande wa usafirishaji ndivyo ufumbuzi wa baadhi ya changamoto zinavyozidi kupatiwa majibu, kama ilivyo kwa Tanzania ilivyoleta mabasi yaendayo haraka ili kuepuka foleni, ndivyo hivyo imetokea Beijing China ambapo wao wameweza kutengeneza basi la umeme lenye uwezo wa kupita juu ya magari mengine.
Kutokana na China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi Duniani, hivyo basi hilo linalotajwa kubeba watu 1200 kwa mara moja, linatajwa kuwa ufumbuzi sahihi wa msongamano wa magari barabarani, basi hilo lilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza May 19 2016.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii