Thursday, May 26, 2016

VIDEO: Mbunge wa Karagwe bungeni na sababu za Wanaume kutooa Wanawake wazuri jimboni

Katika zile stori zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii saa kadhaa zilizopita ni pamoja na hii ya mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa aliyesimama bungeni Dodoma kuchangia bajeti ya wizara ya maliasili na utalii, ishu kubwa ikawa ni kwanini Wanaume wengi jimboni kwake hawaoi Wanawake wazuri?
Kuna changamoto kwenye kata ya Bweranyange sisi tupo kwenye Wilaya iliyopo mipakani, kuna kambi ndogo ya Jeshi. Wananchi wangu wananipigia simu wanalalamika kwamba wanaogopa kuoa Wanawake wazuri kwasababu wanahofia watanyang’anywa na Wanajeshi
Pia Bashungwa ameiomba serikali kuhakikisha inaimarisha ulinzi kwenye kata yaBweranyangi ambako wanajeshi wengi hulinda mpaka wa nchi, ukihitaji kumtazama alivyoongea bonyeza play kwenye hii video hapa chini….

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta