African Sports na Mgambo JKT zote zilikuwa zikihitaji ushindi kwenye mechi zao za leo huku zikiombea mabaya timu za Ruvu JKT na Kagera Sugar ili zenyewe ziwe na uhakika wa kusalia VPL.
Lakini mabo yalikuwa tofauti baada ya Ruvu JKT kuichapa Simba kwenye uwanja wa taifa huku Kagera Sugar wakipata sare ya kufungana bao 2-2 dhidi ya Mwadui FC.
Kwenye uwanja wa Azam Complex, Mgambo imeshuka daraja kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC. Mgambo iliyokuwa ikihitaji ushindi kwenye mchezo wa leo imejikuta ikishindwa kupata ushindi kwa mara nyingine mbele ya Azam ambao sare hiyo imewafanya wamalize kwenye nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga.
Simba waliokuwa wakiwania nafasi ya pili wamechapwa na Ruvu JKT na timu hiyo iliyo chini ya kocha wa zamani wa Simba King Kibadeni imenusurika kushuka daraja.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii