Akizungumza na Ijumaa, nyota huyo ambaye pia hufahamika kama Shishi Baby, alisema maneno ya watu juu ya jambo hilo siyo sahihi, kwani historia ya maisha aliyopitia ndiyo inayomfanya aonekane mkubwa, wakati yeye ni binti mdogo aliyezaa mapema.
Aidha, mkali huyo wa kibao cha Paka la Baa, alisema yeye hivi sasa ana umri wa miaka 30, ‘size’ kabisa kwa wanaume anaotoka nao kimapenzi, kwani hata hao nao, siyo watoto ‘kihiiivyo’ kama maneno ya watu yanavyosema.
Sababu nyingine ni;
.
1: KUOGOPA KUZEESHWA
“Mimi ni kijana kutembea na wazee siwezi, naweza kujikuta nimezeeshwa bure kitu ambacho sikitaki hata kukisikia, kwani naamini bado nina uhitaji kama kijana.
“Angalia wasichana wengi wadogo wanaotoka kimapenzi na wazee hujikuta nao wanakuwa na mambo ya kizee, unadhani atafanya nini wakati ameshakubali kuzeeshwa?”
2: HATAKI KUBURUZWA
“Mimi napenda kuchakarika ndiyo maana sipendi kabisa penzi la wazee ambao ukiwa tegemezi kwao wanakuburuza. Wanawake wengi wanaotoka na wazee huwategemea kwa sababu ya uvivu wao wa kutafuta, kwangu mimi kazi tu!
3: ANASAKA PENZI LA KWELI
“Wasichana wengi wa mjini wamekuwa wakijiingiza kwa wazee lakini hawana mapenzi nao ya kweli, wanakwenda kuchuna pesa kisha wana viserengeti, mimi mwenzao nafuata penzi kwa hao vijana, wanajua kupenda na kwa sababu hobi yangu ni wao siwezi kuwa na wazee kwa kweli.”
4: VIJANA WANA NGUVU, WANAVUTIA
“Na uweke pia hii, kwamba vijana wana nguvu, damu changa na wanavutia, siwezi kutoka na wazee hawana mvuto.”
Baada ya kutaja sababu zake hizo, Shilole alihoji ni yupi mwenye afadhali kati yake na wasichana wenzake wanaotoka na wazee lakini wakiwa wavivu kutafuta?
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii