Thursday, May 12, 2016

Shilole: Najua Kuongea Vizuri Kiingereza ila Napenda Kuongea Kingereza Kibovu ili Kuchekesha Watu

Msanii wa Bongo fleva Shilole a.k.a Shishi Baby amekiri kwamba kuzungumza lugha ya kingereza ni kipaji na wala si hivi hivi tu na amesema yeye anajua kuongea vizuri kingereza ila anapenda kuongea kingereza kibovu ili kuchekesha watu tu.

Na hii ni baada yakuonekana katika mitandaoni mbalimbali ya kijamii akijaribu kwa juhudi zote bila mafanikio kuzungumza lugha hiyo huku ikibaki kuwa kama burudani kwa watu wengine.

“Si munaonaga wenyewe muda mwingine nisipoongea kiswangilishi changu watu wanaanza kunitafuta shishi plizi ongea bhana tunataka uongee”,alisema Shilole.

eatv.tv

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta