Wednesday, May 25, 2016

PICHA; CHUMBA CHA MAAJABU KILICHOPO JUU YA DUNIA

Pichani ni mafundi wakiendelea kumalizia ujenzi wa chumba hicho.
Sayansi ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali Duniani kutokana na staili ya aina yake walivyokitengeneza kwa kutumia  vioo vilivyozunguka kichumba hicho kidogo  hivyo kumuwezesha mtalii kuona kama vile yupo juu ya Dunia.
Unaambiwa sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani  umbali wa  mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila chenji

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta