Wednesday, May 11, 2016

Mwigizaji Lulu Michael Agonganisha Mabwana Wawili Nigeria...Stori Nzima Nimekuwekea Hapa


Ustaa una mambo! Pamoja na kuchukua tuzo na heshima kedekede, Ijumaa Wikienda limetonywa upande wa pili wa ‘shilingi’ ambapo inadaiwa kuwa, Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ aligonganisha mabwana wawili katika hafla ya utoaji wa Tuzo za African Magic Viewers Choice (AMVCA) ililofanyika hivi karibuni nchini Nigeria.

WALISHINDA WABONGO WAWILI
Lulu na mwigizaji Single Mtambalike ‘Richie Richie’ walikuwa ni Watanzania pekee waliokwenda nchini Nigeria na kutunukiwa tuzo hizo ambapo Lulu alishinda kupitia Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki huku Richie akiibuka kifua mbele kwa ushindi wa Filamu Bora ya Kiswahili Afrika Mashariki (Kitendawili).
kiba na lulu tuzoLulu na staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba.

CHANZO CHAVUJISHA MCHAPO
Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo, kilipenyeza habari kuwa, Lulu, pasipo kujua, alijikuta amegonganisha mabwana wawili, staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba na bosi mmoja wa redio yenye jina kubwa Bongo (jina tunalihifadhi kwa sasa).
“Si unajua Kiba naye alikuwa bado ana matumaini na Lulu maana wametoka mbali. Kiba alijua kwamba kwa kuwa alialikwa kutumbuiza, basi ingekuwa rahisi kuwa ‘klozi’ na Lulu baada ya kupewa taarifa kwamba Lulu naye anakwenda.
“Akaibuka mazima pasipo kujua kuna mtu mwingine ambaye ndiye anasimamia mpango mzima wa Lulu kwa sasa. Kuanzia mavazi hadi malazi, achilia mbali mazagazaga ya kila siku.
luluLulu alivcyopokelewa Tanzania.

BOSI WA REDIO FULL KUSIFIWA
“Bosi wa redio si unajua tena yeye nd’o mwenyewe? Full kujiamini. Hakuwazia kabisa kama kuna mtu mwingine anaweza kuwa na nafasi kubwa kwa Lulu kama ilivyo yeye. Si unajua tena kasimamia shoo nyingi tu hadi ya kuhamasisha watu kumpigia kura Lulu?

KIBA AAMBULIA HOTELINI
“Kiba alipata bahati ya kukutana na Lulu kwenye Hoteli ya Eko ilipofanyika hafla ya utoaji wa tuzo hizo wakapiga picha ya pamoja lakini baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo, mtoto mzuri alikamatiwa na the big boss wa redio, wakaenda zao kulala,” kilisema chanzo hicho.

BOSI WA REDIO NI NANI?
Katika kumwaga ubuyu, chanzo hicho kilizidi kumdadavua bosi huyo wa redio ambaye ndiye aliyeshikilia ‘mpini’ siku hiyo kwani Lulu hakuweza kupata muda hata kiduchu wa kukutana na Kiba tofauti na pale ukumbini.

“Kwani unafikiri bosi mwenyewe ni nani basi, si ni (anamtaja jina) ambaye kama mnakumbuka vizuri alikuwa mchumba wa yule Video Queen wa Bongo, Hamisa Mobeto, Lulu akampora. Bosi kubwa hakumpa nafasi Lulu hata kidogo ya kutembea,” kilisema chanzo hicho.

KIBA AREJEA BONGO KIVYAKE
Vyanzo mbalimbali vya habari vilitonya kuwa, Kiba alirejea Bongo kivyake huku Lulu akiwasili jijini Dar akiwa sambamba na watu wake wa karibu akiwemo bosi huyo wa redio.

BOSI ANASEMAJE?
Baada ya ya jitihada za kumtafuta Kiba kugonga mwamba, gazeti hili lilimvutia waya bosi huyo wa redio ili kutaka kumsikia anazungumziaje kitendo cha yeye kuonekana kule huku pia mwanaume aliyetajwa kutembea na Lulu zamani (Kiba) akiwepo, bosi huyo hakutaka kuzungumzia chochote.
“No comment.”

LULU ASAKWA, KIMYA!
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumsaka Lulu ili kuzungumzia suala hilo lakini hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, bado hakujibu chochote.

SHOSTI WAKE AKIRI
Hata hivyo, rafiki mmoja wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina, alikiri Lulu kuwa na bosi huyo kama mpenzi wake wa sasa lakini akampa pole Kiba.
“Huyo bosi ndiyo mtu wake, alikuwa na haki ya kwenda na Lulu kule na kuwa na uhuru wa kila kitu lakini Kiba ni rafiki na mdau mkubwa wa sanaa alienda kufanya shoo,” alisema shosti huyo.

Chanzo:Global Publishers

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta