Wednesday, May 25, 2016

Msanii CHID BENZ Adaiwa kutoroka SOBER HOUSE...!


Wakati wadau wa muziki wakifahamu kuwa msanii wa Muziki wa Hip Hop nchini, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ yuko katika kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya ‘sober house’ kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani, inadaiwa jamaa alishatoroka kitambo na sasa yuko kitaa. 

Habari zinadai kuwa Chid alitoroka kituoni hapo baada ya kushindwa kuhimili mazingira yalikuwepo hivyo akaona bora arudi mtaani baada ya kuonesha dalili za kuchokaa kuishi maisha ya kituoni hapo. 

Kwa mujibu wa meneja wa kituo hicho, Tumaini Majura ambaye amethibitisha kuondoka kwa Chid akiwa bado anaendelea kupatiwa matibabu amedai kuwa Chid ameishi kituoni hapo kwa muda wa siku 28. 

Amedai kuwa Chid, alikuwa naonesha kuchokaa maisha ya kituoni hapo kwani alikuwa anagoma kufanyia usafi na muda mwingi aliutumia kulala na kuandika mashairi na wakati mwingine kuwahimiza wenzake kugoma katika vitu fulani. 

Amedai kuwa mara mwisho Babu Tale kwenda kumuona msanii huyo aligoma kabisa kubaki kituoni hapo na kumtaka kuondoka naye, lakini Tale, alimsihi sana kuwa mvumilivu walau abaki kwa miezi mitatu kabla ya kuanza kufanya shoo. 

Alipotafutwa Tale, kuhusiana na madai ya Chid kutoroka amedai kuwa kwa sasa hataki kusikia habari hizo lakini muda ukifika ataliweka wazi jambo hilo.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta