Wednesday, May 11, 2016

HAWA ALIYE IMBA YIMBO YA NITAREJEA NA DIAMOND AFUNGUKA MENGI JUU YA MAISHA YAKE..MSIKIE

Msanii Hawa ambaye aliimba na Diamond kwenye wimbo wa nitarejea, amesema kwa sasa mume wake ndiye mtu muhimu zaidi maishani mwake kwani amembadilisha maisha yake.

Hawa ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa wakati anakutana na mume wake huyo ambaye anadaiwa kumbadilisha mpaka dini na kuwa mkristo, alikuwa kwenye hali mbaya kwa ulevi.

“Mume wangu ndio kitu kikubwa sana kwa sababu kanibadilisha katika njia nyingi sana, kipindi ambacho nalewa kwa sababu nilikuwa sikumbuki hata kuoga watu wananisema kabisa huyu kawa teja, sikumbuki kufanya kitu chochote mi nakumbuka kulewa tu lakini Lordvick alijitajahidi kwa ahali yoyote kunifanya mimi nionekane katika hali ya usichana, na nilijisikia vizuri nikahisi yeye ndo ananifaa”, alisema Hawa.

Hawa ambaye kwa sasa bado anaendelea na shughuli za muziki na hivi karibuni alikiri kuhitaji uongozi wa kumsimamia kazi zake, amesema yupo na mume wake huyo kwa ajili ya upendo aliounyesha na kumjali, lakini si pesa.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta