Wcb staa Harmonize amesema alimkuta mpenzi wake Jackline Wolper akiwa single, ndiyo maana wakaweza kuanzisha mahusiano.
Harmonize amesema hayo kupitia kipindi cha Enews ambapo alikuwa anaelezea mambo mbalimbali kuhusu maisha yake mapya katika mahusiano na Wolper ambaye yeye mwenyewe amekiri kuwa ni mtu aliyeanzisha naye mahusiano hivi karibuni na kusema tuwe na subira kila kitu kitakuja kuwekwa wazi siku za usoni.
“Unajua mpaka saizi sijamvisha mtu pete ya uchumba wala mimi sijawahi kuvishwa pete ya uchumba ila niseme tu ni kweli nipo kwenye mahusiano na Wolper ambaye ni maarufu kama mimi na wakati ukifika kila kitu kitawekwa wazi” alisema Harmonize
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii