Saturday, May 28, 2016

Gigy Money sikio la kufa

KUONESHA kwamba haoni wala hasikii, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amezidi kutia fora kwa kunaswa na wanaume tofauti safari hii, ametupia picha kimahaba akiwa na msanii wa Singeli, Amani Fongo.
gadner&gigyGigy ambaye amekuwa akitupia picha za nusu utupu katika Mtandao wa Instagram pamoja na kuwa kimahaba na wanaume tofauti kama staa wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’, mtangazaji Gardner G. Habash na Idris Sultan, amepondwa vibaya baada ya kutupia picha mpya ya Fongo.
gigy na nay3“Huyu kama vile hana wazazi sasa tumueleweje, mara Gardner mara Matonya yaani sijui ndiyo kiki au vipi,” aliandika mdau mtandaoni huku Gigy mwenyewe akidai aachwe kwani ndiyo maisha yake.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta