Sunday, May 15, 2016

Faiza Asaka wa Kumpa Penzi, Wanaume Kazi Kwenu

Staa mrembo kutoka Bongo Movies,  Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’ ametoa kali baada ya kusema kuwa ana hamu ya kumpata mwanaume mwingine wa kumpa raha lakini mpaka sasa hajapata.

Akizungumza na  gazeti la Ijumaa juzikati, Faiza alisema tangu alipoachana na Mheshimiwa Sugu, aliona bora ajitulize lakini sasa anajiona kuna kitu anakikosa na wa kumpa kitu hicho ni mwanaume.

Niseme tu kwamba tangu niachane na Sugu sijakutana na mwanaume mwingine, hebu ‘imagine’ ni muda gani? Sasa nimeshindwa kuvumilia, natafuta wa kunipa raha maana kuna hali flani ikinijia nakuwa kama chizi, swali ni je, nani mwanaume sahihi wa kunipa ‘zawadi’ hiyo? Hapo ndipo mtihani ulipo,” alisema Faiza.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta