Ofisa habari wa Yanga Jerry Muro amesewaomba radhi mashabiki na viongozi wa Simba kutokana na maneno ambayo alikuwa akiyatumia wakati wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikiendelea.
Muro amesema inawezekana kuna baadhi ya mashabiki na viongozi wa Simba walikuwa wakikwazwa kutokana na maneno yake kupitia vyombo vya habari hivyo ameamua kuomba radhi wakati ligi hiyo ikielekea kumalizika May 22.
“Najua kwenye msimu mzima wa ligi tumekwazana sana na kunawatu watakuwa wameumia sana kuhusu maneno yangu,lakini mimi nilikuwa kazini nikitetea ajira yangu na mkate wangu ambao nimeutetea na nimeupigania kikamilifu”, anasema msemaji huyo wa Yanga baada ya timu yake kufanikiwa kutwaa taji la VPL kwa msimu wa pili mfululizo.
“Nimetimiza jukumu langu la kuhamasisha wanayanga kutengeneza morali kwa timu hadi tumechukua ubingwa. Sasa kazi imeisha turudi kuombana radhi, wale ambao walikuwa wanaguswa na maneno yangu niwaambie tu yamekwisha, tusameheane, yalikuwa ni maneno tu yakuleta chagizo kwenye mchezo wa mpira wa miguu wala hayakulenga kutukanana wala kuleta uhasama”.
Muro amekuwa akitumia majia tofauti kuiita klabu ya Simba majina ambayo yamekuwa yakiwaudhi mashabiki wa Simba. ‘Wamchangani’, ‘wamatopeni’, ‘Wazee wa Youtong, ‘Vyura FC ni baadhi ya majina ambayo msemaji huyo wa Yanga amekuwa akiwalenga Simba.
Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii