Tuesday, May 17, 2016

Elewa faida lukuki za kula bamia

LadiesFinger5
Chimbuko la bamia ni Ethiopia kisha ikaenea duniani kote. Unafahamu kwa kula bamia unaweza ukawa umejiondoa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali mwilini?
Mtandao wa Healthandcure.com unawanukuu wataalam wa afya wakieleza kuwa watu wanaosumbuliwa na maradhi ya mfumo wa chakula kama vile vidonda vya tumbo na mengine yanayofanana na hayo wanaweza kupata ahuweni au kupona kabisa ikiwa watakula bamia.
Wataalam hao wanaendelea kuzitaja faida nyingine zinazotokana na ulaji wa bamia ni pamoja na kuboresha uwezo wa macho kuona.
Bamia ni chanzo kizuri cha Vitamin A na Beta Carotene ambavyo ni virutubisho vinavyosaidia kuboresha uwezo wa kuona.
Bamia inasaidia kuweka kawaida kiwango cha sukari mwilini na nyuzinyuzi zake zinasaidia kurahisisha ufyonzwaji wa sukari mwilini.
Michirizi na utomvu unaopatikana katika bamia, husaidia kusawazisha sukari mwilini kwa wagonjwa wa kisukari kwa kuzuia kiwango cha sukari inayotumika katika mwili kutoka kwenye utumbo mkubwa.
Pia hudhibiti kiwango cha lehemu mwilini na hasa pale inapokuwa mtu ametumia vyakula vingi vyenye mafuta. Husaidia pia kulainisha choo.
Vilevile bamia ni mboga ambayo kwa Waafrika huongeza hamu ya kula na hata kurahisisha kazi ya kumeza chakula.
Wataalam wanaeleza kuwa ina virutubisho vinavyoweza kupambana na bakteria wanaoshambulia utumbo na kusababisha vidonda vya tumbo.
Pamoja na haya yote bamia huimarisha mifupa, huongeza kinga dhidi ya magonjwa ya figo, saratani pamoja na pumu. Utelezi wake huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali Cholesterol na asidi ya nyongo unaoingia kutoka kwenye ini ambao usipodhibitiwa huenda ukasababisha matatizo ya kiafya.
Bamia husaidia kulainisha utumbo mkubwa Large Intestines kutokana na kazi yake ya kulainisha choo hivyo huzuia kufunga choo.
Bamia ina Vitamin C ambayo inawafanya watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe ya bamia iliyopikwa huwa na miligramu 13 ya vitamin C.
Bamia husaidia kuweka utumbo kuwa na hali nzuri hivyo kupunguza uwezakano wakuugua ugonjwa wa kansa hasa kwenye utumbo mkubwa. Pia kula bamia kwa wingi kunasaidia kuimarisha mishipa midogo ya damu.
Nusu kikombe cha bamia iliyopikwa inakua na kiwango cha 460 IU ya vitamin A ambayo inapunguza uwezakano wa kupata ugonjwa wa mtoto wa jicho Cataracts.

Tupe Maoni Yako Kuhusu Habari Hii

 

GOSSIPS Copyright © 2016 -- Template created by Mbatta